Header Ads Widget

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DKT. PINDI CHANA AKUTANA NA WATAALAMU WA IDARA YA WANYAMAPORI JIJINI DODOMA

 



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana leo tarehe 05 April, 2022 amekutana na Wataalamu kutoka Idara ya Wanyamapori kwa lengo la kupata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya Sekta ya Wanyamapori nchini .





Katika Kikao hicho Waziri Dkt.Pindi Chana amewasisitiza watalaam hao wafanye kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ili kuboresha Sekta hiyo kwa kuvutia Watalii na kuongeza Pato la Taifa hususani katika kipindi hiki ambacho tasnia ya utalii imeathiriwa na janga la UVIKO 19.




Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi, Mkurugenzi wa Idara ya  Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha pamoja na Wataalamu mbalimbali kutoka idara ya Wanyamapori.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI