LEO Tanzania na Misri zimesaini Mkataba wa kuzalisha na kuuza mazao ya kilimo hususani Mahindi ya Njano, Meupe, Soya, na Ngano. Mkataba umesainiwa na ndugu Revocatus Kimario Mkurugenzi wa SUGECO kwa upande wa Tanzania na Smart Group Import & Export Company Ltd, ya Misri. Kwa mkataba huu wakulima sà sa wana uhakika wa masoko ya mazao yao.
Mkataba huu umesainiwa katika ubalozi wa Tanzania nchini Misri ukishuhudiwa na Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, in balozi wa Tanzania nchini Misri.
Aidha mkataba huu umeshihudiwa na Dr. Fulgence Mishili vice Chair SUGECO Board, Dr. Juliana Mwakasendo Mkurugenzi wa uhawilishaji wa teknolojia na mahusiano wa TARI na Bi. Jack line Shayo Mkurugenzi wa Maendeleo ya biashara kutoka ASA.
Kwa mkataba huu Tanzania imepata fursa ya kuzalisha na kuuza mahindi zaidi ya tani milioni 1.5 kwa mwaka. Pia tumepata fursa ya kupata mbegu Bora.
Aidha SUGECO watafanya kazi na TARI, ASA na TOSCI ili kuzalisha mbegu hizo nchini Tanzania.
Thamani ya mkataba huu kwa mwaka ni zaidi ya bilioni 820 na huu ni mkataba wa miaka 5.
0 Comments