Header Ads Widget

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA ENEO LA MRADI WA LNG

 




Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ametembelea na kukagua eneo la Likong'o litakalojengwa Mradi wa kusindika Gesi Asilia (LNG) na eneo la makutano ya kuunganisha gesi inayotoka mkoa wa  Mtwara na Songosongo mkoa wa Lindi.



Akiwa katika ziara hiyo amewaasa watendaji wa maeneo hayo kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.



Katika ziara hiyo ya kikazi, Mahimbali aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Kamishna Msaidizi wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Mohamed Fakih, na Meneja wa Kiwanda cha kuchata gesi asilia cha Madimba, Mhandisi Sultan Pwaga, pamoja na maafisa wengine kutoka wizarani na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Ziara hiyo imefanyika Aprili 2, 2022 mkoani Lindi.





Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara yake aliyoianza Machi 31, 2022 kwa kukagua mradi wa gesi wa Songosongo mkoani Lindi, kisha Aprili 1, 2022 alikagua kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, visima vya gesi katika eneo la Mnazi Bay pamoja mradi wa usambazaji wa miundombinu ya gesi asilia kwa matumizi ya kupikia majumbani.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI