Header Ads Widget

SERIKALI YA UINGEREZA YAZINDUA MRADI WA SHULE BORA

 


SERIKALI ya nchi ya Uingereza imezindua mradi wa Shule Bora unaohudumia watoto milioni nne kwenye mikoa tisa hapa nchini.


Akizindua mradi huo kwenye Shule ya Msingi Mkoani Halmashauri ya Mji Kibaha

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibiani Vicky Ford amesema mradi huo ni kuhakikisha  watoto wanakwenda shule kwa muda uliopangwa hasa wa kike 


Ford alisema kuwa serikali ya Uingereza imeamua kuwekeza kwenye sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto kupata elimu bora.


Amesema kuwa mradi huo wa elimu na utawajengea uwezo walimu huku watoto wote pamoja na wenye mahitaji maalumu wanakuwa shule ambapo nusu ni wa kike kuwa shuleni kubaki kwa muda unaotakiwa.


Naye Waziri wa Elimu  Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa  mradi umefadhiliwa na Uingereza kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na kuhakikisha wanafunzi wanaingia madarasa na kusoma na  kuboresha ufundishaji madarasani.


Mkenda alisema kuwa pia ni kuwawezesha walimu waweze kuboresha ufundishaji na unaendana na azma ya serikali kuboresha elimu nchini ili iwe na ubora mikoa hiyo ni Pwani, Katavi, Kigoma, Mara,Tanga, Dodoma, Singida, Rukwa na Simiyu.

Naye mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema wanashukuru kwa kupewa mradi huo watautunza na kuuangalia vizuri sana ili ulete manufaa kwa wananchi wa mkoa wa Pwani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI