Header Ads Widget

MTOTO WA MIAKA 15 ALAWITIWA AKITEKA MAJI BWAWANI

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MWANAFUNZI wa kiume  wa kidato cha kwanza mweye umri wa Miaka 15 anayesoma katika shule ya sekondari Chikole iliyopo mkoni Dodoma amelawitiwa na  Mwanaume mwenye umri wa miaka kati ya 35-40 wakati akiteka maji kwenye Bwawa kwaajili ya kusafisha darasa


Tukio hilo limetokea mnamo Aprili 1,2022 majira ya saa 6:00 mchana katika Bwawa mtaa wa Senje Kata ya Msalato mkoani hapa.


Akizingumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Onesmo Lyanga amesema mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo baada ya kuwakamata wanafunzi watatu walio kuwa wakichota maji kwa ajili ya usafi wa darasa huku akiwatishia  kuwaua kwa panga kisha kumlawiti mmoja wao.


‘’Kwa bahati mbaya walikuwa wanafunzi sita walikuwa wameenda kuchota maji  katika hilo Bwawa na wakaweza kukutana na mtu mmoja ambaye wao wanamtambua kwa sura na waajiri wake. 


Na kuongeza "Mtu huyo ameweza kuwatolea vitisho na kuwauliza maswali,kwanini wanateka maji hapo? na akawauliza wale ambao ni mara yao ya kwanza kuteka maji katika Bwawa hilo wakatokea wanafunzi watatu wakamjulisha kwamba wao ni mara yao ya kwanza akawaambia nyinyi nendeni .’’ amesema Lyanga


Amendelea Kusema"Lakini akawachukua wanafunzi watatu  huku akiwa na kitu kama panga na kuwatisha baada ya kufanya hivyo aliwachukua na Kwenda nao  katika vichaka na ndipo huko alipo weza kufanikiwa kumlawiti mwanafunzi mmoja kati ya hao watatu.’’ amesema Lyanga


Aidha, Lyanga amesema mhanga wa tukio hilo kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma 


"Uchunguzi zaidi unaendelea wa kumtafuta mtuhumiwa na kumbaini Lakini niagize na kumtaka mtuhumiwa ajisalimishe haraka kwa kuwa anatambulika kwa sura.’’ anasisitiza Lyanga


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI