Header Ads Widget

MANGE KIMAMBI AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUACHIWA WAFANYAKAZI WAKE, ATOA NENO

Ahsante Kwa kuchagua Matukio DaimaAPP ,Karibu Sana ujiunge na familia ya Matukio Daima Media Kwa kupakua APP ya Matukio Daima kupitia Google Play store ni bure kabisa kupitia App hii utaweza kuunganishwa na habari zinazotolewa na media zetu ikiwemo blog , Instagram, Twitter na Online Tv karibu Sana pia Kwa huduma ya matangazo na habari wasiliana nasi Kwa simu 0754 026 299



Na Matukio Daima APP, DAR

JESHI la Polisi limewaachia kwa dhamana wafanyakazi wawili wa Mtandao wa Mange Kimambi App waliokuwa wakishikiliwa na jeshi hilo tangua Machi 14, mwaka huu kwa kosa la kurusha maudhui yasiyofaa mtandaoni.

Kuachiwa huko inakuja baada ya juzi Mwanadada huyo kubandika walaka mzito Rais, Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya kuendelea kushikiliwa wafanyakazi wake hao bila kupelekwa Mahakani huku akibainisha kuwa, tukio wanaloshikiliwa lina dhamana.

Mapema mchana wa leo, Aprili Mosi, mwanadada huyo amebandika ujumbe juu ya kuachiwa kwa wafanyakazi hao huku akimshukuru Rais Mhe. Samia kwa hatua hiyo.

Bandiko la taarifa hiyo alilobandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram ya mangekimambi_

‘’Alhamdullilah, Mungu ni mkubwa. Finally vijana wameachiwa mchana huu.

Sitoongea mengi. Ila ahsante Serikali yangu. Ahsante Rais wangu. Haki imetendeka, vijana wamepewa haki yao ya dhamana.’’ Ameandika Mange Kimambi.

‘’Ila Chama cha mapinduzi na Serikali kwa ujumla mna kazi kubwa sana ya kufanya juu ya Polisi na utendaji wa haki. 

Haki ya dhamana bado ni shida kubwa Tanzania. Haki ya dhamana inatakiwa iwe ‘automatic’ na sio mpaka mtu aje kumlilia Rais kwenye ‘social media’ ndio dhamana itolewe.

Sio kila mtu ana ‘platform’ kama hii. Na pia Rais ana mambo mengi ya msingi ya kufanya, kweli ataweza kufatilia mtanzania yupi kanyimwa haki ya dhamana? Pia sio kila mtanzania ana pesa ya kulipa mwanasheria. 

Je watanzania wasio na uwezo nani anawapigania kwenye swala la kupata dhamana? Si wanaozea polisi ama Segerea?’’ Aliandika Mange Kimambi

‘’Yani toka nimeposti hii issue juzi nimepokea malalamiko mengi ya watu wanaomba niposti ndugu zao wanaoshikiliwa na polisi bila dhamana na wakati kesi zao zina dhamana watu wengi mno

Je nani anawasaidia hawa? CCM fanyeni kitu hapa. Inabidi kuwe na complete overhaul ya polisi nzima.’’ 

Mzee Kinana nakuaminia kuwa kuna jambo utafanya kupush changes juu ya polisi maana wanachafua serikali na chama kizima kwa uonevu wao.’’ Alimalizia Mange Kimambi.

Wafanyakazi hao wawili walioachiwa leo kwa dhamana ni pamoja na Meneja wa Mange Kimambi App, Bw. Allen Mhina ambaye ni mdogo wa Mange Kimabi pamoja na Binti wa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Clouds Media Group, Sakina Lyoka, aliyefahamika kwa jina la Rehema Lyoka maarufu kama Reytox ambapo wafanyakazi wengine 11 waliachiwa  toka awali.

Jeshi la Jeshi la Polisi lilikuwa likiwashikilia kwa kile kilichoelezwa matumizi mabaya ya mitandao ambapo ilidaiwa kuwa walirusha maudhui ya video ya Msanii na Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA], ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay.

Maudhui hayo yalidaiwa kuwa yalionesha Prof. Jay akiwa kitandani chumba cha wagonjwa mahututi [ICU] hali ambayo ilileta taharuki kwa ndugu wa mgonjwa, Madaktari na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amelazwa na kupatiwa matibabu.

Mtandao huu wa Matukio Daima ndo ulikuwa wa kwanza kuripoti juu ya tukio la kukamatwa kwa wafanyakazi hao wa Mange Kimambi App zaidi ya 10, ambapo hata hivyo awali Jeshi la Polisi halikuwa wazi kusema hadi pale Mwanadada huyo kuandika kwenye kurasa wake ndipo taarifa ya jeshi ilitoka kwa umma juu ya kuwashikiria wafanyakazi 13 pamoja na vifaa vya ofisi mbalimbali zikiwemo camera, Laptop, na vingine vingi vya Kimawasiliano.

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI