Header Ads Widget

KAZI YA UKUSANYAJI MAPATO YA MIRABAHA YAKABIDHIWA MIKONONI MWA SUMA JKT

 



Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Taasisi ya Hakimiliki Tanzania COSOTA leo imeingia mkataba na Kampuni ya SUMA JKT  Auction Mart Ltd kwa ajili ya ukusanyaji wa mirabaha katika Mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma, huku ikiwa kwa Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro kuna wakala ambae anasimama kwa niaba ya Cosota ambae ni Tanzania Finance Corporation.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa  Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Philemoni Kilaka wakati wa kutia saini makubaliano na kampuni hiyo ya SUMA JKT Auction Mart Ltd amesema kuwa utaratibu wa ukusanyaji wa ugawaji wa mirabaha unafanyika sehemu mbalimbali za kazi duniani.


Amesema kuwa, ni kosa la jinai kwa mtumiaji wa kazi za sanaa katika maeneo mbalimbali ya biashara kutumia kazi hizo bila kulipia matumizi ya kazi hiyo COSOTA au kupata kibali kwa msanii mwenyewe, adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi cha shill 20,000,000.


Aidha, amesema Ili kuhakikisha  adhma ya serikali inatimia kwa wasanii kuendelea kunufaika na mirabaha wataendelea kuingia mikataba katika sehemu mbalimbali Ili kuongeza makusanyo kwa kuyafikia maeneo mengi.


Hata hivyo, ametoa kwa watumishi wote wa kazi za muziki na FILAMU nchini katika maeneo ya kibiashara kuhakikisha wanalipia matumizi ya kazi hizo Cosota Ili kuepusha usumbufu pale zoezi la oparesheni ya ukaguzi litakapofanyika.


Kwa upande upande wake,  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji SUMA JKT Meja Jamal Juma Mohammed amesema wasanii wanahaki ya kufaidika kama watu wengine wanavyo faidika na kazi zao, hivyo wamejipanga kuhakikisha mapato yote yanakusanywa kwa watu wote wanaopiga kazi zao.


Naye, Mwanasheria wa COSOTA Zefania Lyamuya amesema kazi ya kukusanya mirabaha inataratib makubaliano walioingia ni ya mwaka mmoja na muda wa matazamio ni miezi mitatu. 


"Mkataba ni kukusanya mirabaha tumewapatia mafunzo kwaajili ya ukusanyaji tumeanza na mikoa hii miwili tutakwenda nao mikoa mingine ili kuhakikisha pesa za mirabaha ya wasanii haipotei.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI