Header Ads Widget

WAKAZI WA RUVUMA WATAKIWA KUZINGATIA ULAJI WA VYAKULA WA MAKUNDI MATANO.



 Na Amon Mtega_   Songea.



KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru taifa Sahili Nyanzabara Geraruma amewataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kuzingatia ulaji wa vyakula kwa kuzingatia makundi matano ili kutokomeza udumavu ambao umekidhili baadhi ya mikoa hapa Nchini.

 

 Wito huo ameutoa wakati mwenge ukikagua mradi wa Lishe  uliyopo Kijiji cha Lipokela katika Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma ambapo miradi nane ilikaguliwa kwa kuizindua  na mingine kuiwekea mawe ya misingi.


Geraruma amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya watu kushindwa kuzingatia ulaji wa vyakula vya makundi matano jambo ambalo limekuwa likisababisha kuendelea kuwepo kwa udumavu hasa kwa watoto.



Kiongozi huyo licha ya kuwataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kula vyakula vya makundi matano laki bado amewataka kutumia vyandarua kikamilifu ili kutokomeza malaria ambayo nayo bado yamekuwa tishio kwa jamii.



Katika hatua nyingine kiongozi huyo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuwa na miradi mizuri ambayo yote imekubaliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru.

 


 Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya ya Songea Joyce Kamanga amesema kuwa kituo hicho cha lishe kimekuwa kikitoa Elimu kwa Wananchi juu ya matumizi sahihi ya ulaji wa vyakula kwa kuzingatia makundi matano.

       

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI