Header Ads Widget

ZEBAKI NI MIONGONI MWA VYANZO 10 HATARISHI KWA AFYA YA BINADAMU

 .


SHIRIKA  la Afya Duniani (WHO), limeitaja Zebaki kuwa ni miongoni mwa vyanzo 10 hatarishi kwa afya ya binadamu ambapo kutokana na hali hiyo, Jumuiya ya kimataifa ilipitisha Mkataba wa Minamata mwaka 2013, wenye madhumuni ya kulinda afya ya binadamu dhidi ya madhara ya uchafuzi wa mazingira unaotokana na kemikali hiyo.Mwandishi Hamida Ramadhan MDTV  Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Edward Nyamanga amesema hayo leo Machi 15 2022  jijini Dodoma wakati akifungua Warsha ya Uhamasishaji wa Utekelezaji wa Mpango – kazi kitaifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwenye Uchimbaji mdogo wa Dhahabu (2020-25).


Nyamanga amesema sekta ya wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini hutumia tani 18.5 za Zebaki kila mwaka bila kuzingatia tahadhari kiasi kinachoweza kuathiri afya za wananchi na mazingira hali inayoweza kuathiri ustawi wa maendeleo endelevu ya nchi yetu.


"Licha ya faida kubwa inayopatikana kutokana na sektahii shughuli za wachimbaji wadogo zimeweza kuibua  changamoto nyingi kwa afya ya binadamu na Mazingira zikiwemo umwagaji maji  yenye sumu kwenye mazingira," amesema Nyamanga.


PAKUA APP YA MATUKIO DAIMA KUPITIA GOOGLE PLAY STORE BURE 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI