Adeladius Makwega-DODOMA
Dunia imepambwa kuwa na wanyama mbalimbali, wale wanaoishi na binadamu na hata wale wa misitu. Miongoni mwa wanyama wa msituni ni Simba na Chui.
Wanyama hawa wawili kila mmoja amekuwa na tabia yake ya kujitafutia chakula na namna ya kula chakula hicho. Kwa kuwatazama wanyama hawa wote ni wakali, mabingwa wa kuwinda.
Simba amekuwa na desturi anaweza kukuta kundi la swala, atamtazama mmoja amtakaye ataanza kumsaka,
Cha kustajabisha simba mara zote katika kundi la swala, humkamata na kumuua swala mmoja tu yaani wa chakula cha siku hiyo tu.
Hapo umkamata na kumuua mnyama huyo na kumvuta pahala nakuanza kumla akiwa yeye mwenyewe, watoto wake au simba wenzake waliokuwa kando.
Wanyama wengine wadogo wadogo wanaokula nyama, kama fisi na ndege hujikarisha katika chakula hicho na kula.Windo la simba linawashibisha wengine.
Chui nayeye huwinda kama anavyofanya simba na mara baada ya kupata windo lake hulibeba na kuutafuta mti mrefu na kuhifadhi huko juu, huku akila kwa siku kati ya moja hadi nne.
Nyama inayofichwa huko juu ya mti haiwezi kuwasaidi wanyama wengine kama fisi kwani hawawezi kuupanda mti huo labda vipande vidogo vidogo vinayoanguka kwa bahati mbaya kutoka juu ya mti.
Namna hii ya uwindaji na ulaji wa Simba ndivyo ilivyokuwa ikifanywa na jamii nyingi za Waafrika. Baada ya kuwinda nyama hiyo inagawanywa na kuliwa na wengi hata kama itauzwa au kubadilishana na vitu vingine.
Ndiyo kusema ulaji wa Chui unabebwa na dhana ya ubinafsi lakini ulaji wa simba ni dhana ya umoja na manufaa kwa sote.
Mwanakwetu nakupa Chemsha Bongo kidogo, tazama pahala popote ulipo, alafu chukua karatasi andika maneno mawili kushoto CHUI na kulia SIMBA. Hapo ulipo fafuta watu sita, kwa yule mwenye tabia ya simba muweke kwa Simba na mwenye tabia ya chui mweke kwenye kundi la chui.Ukimaliza watu sita jipime na wewe Je ni Chui au Simba?
Ukimaliza yote, nakushauri kuwa na tabia kama ya SIMBA anavyokula windo lake.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments