Header Ads Widget

WATANZANIA WATAKIWA KULINDA KULINDA AFYA YA VINYWA VYAO KWA KUVIANGALIA KWA WATALAAMU WA AFYA MARA KWA MARA

 


WATANZANIA  wameaswa kulinda afya zao za Kinywa na meno kwa kufuata njia sahii za kujikinga ili kupunguza tatizo la ugonjwa ambalo kwa sasa linaendelea kuwashambulia watu wengi . Mwandishi Amon Mtega, MDTV Songea

 

Hayo yamesemwa  na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Ruvuma.


Prof. Makubi amesema kuwa suala la kujikinga na Magonjwa ya Kinywa na Meno ni muhimu zaidi kuliko kusubiri kuingia kwenye hatua ya matibabu jambo ambalo matibabu yake hutumia gharama kubwa.


"Usafishaji wa kinywa kwa usahihi, matumizi ya miswaki yenye sifa stahiki, na udhibiti wa ulaji wa vyakula vyenye sukari mara kwa mara na kufanya uchunguzi wa Kinywa na Meno walau mara moja kwa mwaka ni miongoni mwa mambo ya msingi na ya lazima ili kuwa na Kinywa chenye Afya njema" amesema Prof Makubi . 



Aidha, amesema matumizi ya sigara na bidhaa za tumbaku pamoja na unywaji wa pombe uliopitiliza huchangia kupata madhara ya magonjwa ya fizi, saratani kwenye ulimi, mdomoni na koo hivyo watumiaji wanatakiwa kujihadhari navyo.


Hata hivyo Prof. Makubi amewahimiza watanzania Kujiunga na mfuko wa bima ya Afya ili kuweza kupata huduma kwa gharama nafuu na haraka.


"Wito wangu kwa Watanzania  tuendelee kujitokeza kwa hiari kujiunga na mfuko wetu wa bima ambao utasaidia kuboresha huduma zetu na kupata huduma bora za Afya " amesema Prof. Makubi


Prof. Makubi amesema Serikali imeendelea kuhakikisha huduma ya Kinywa na Meno zinaimarika, kwa kuendelea kununua vifaa tiba vya kisasa na kuboresha miundombinu ya matibabu hayo katika hospitali na vituo vya afya.


Hata hivyo  Prof. Makubi alimshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha huduma za afya zina imarika kwa kuendelea kununua vifaa vya kisasa, kujenga miundombinu na kuboresha matibabu kwa ujumla.


"Kwenye fedha za Uviko - 19 uwekezaji mkubwa umefanyika katika vituo vyetu vya afya kwa kujenga vyumba vya kutibu wagonjwa mahututi na dharura pamoja na vifaa vya kisasa" amesema Prof Makubi.



 Naye Rais wa Chama Cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno (TDA)Dr.Deogratias Kilasa awali wakati akisoma risala amesema kuwa kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo Wataalamu wa magonjwa ya vinywa walikuwepo Mkoani Ruvuma kutoa huduma ya kinywa na meno ambapo wakazi mbalimbali walitumia fursa hiyo kuangalia vinywa vyao bure.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI