Header Ads Widget

WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI LINDI

Jeshi la Polisi Mkoani  Lindi linawashikilia watu  wanne kwa tuhuma za kukutwa na kilo gram 261 ya  meno ya Tembo  yenye thamani ya shilingi milioni 69.5 , Mkonga 01 wa tembo , vipande 87 vya nyama ya tembo , bunduki moja  aina ya Rifle 375 maganda ya risasi 07  na vichwa vya risasi 06, risasi 01 inayodhaniwa kutengenezwa kienyeji  na mitego ya Waya "Roda" 09 .MWANDISHI HADIJA OMARY MDTV LINDI

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi alisema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 17 mwezi march 2022 huko katika Kijiji cha kiangala kata ya kibutuka Wilayani Liwale Mkoani Lindi

Kamanda Kitinkwi amesema kushikriwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na msako ulioendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na  mamlaka ya Wanyama pori Tanzania (TAWA) katika muendelezo wa kudhibiti vitendo vya ujangili ambapo lilianzisha msako mkali katika Wilaya hiyo ya Liwale



Kitinkwi alieleza kuwa baada ya Mtuumiwa wa kwanza alietambulika kwa jina Moja tu la Mohamedi  kuhojiwa kwa kina baada ya kukamatwa alieleza kuwa tembo hao wawili waliwawinda katika mapori ya Wazi ya Nyera kipelele (TFS) na (Hangai)  Chini ya kijiji yaliyopo kata ya kiangara Wilayani Liwale Mkoani Lindi.


Hata hivyo Kitinkwi alifafanua kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi mpaka pale upelelezi utakapo kamilika kwa ajili ya kufikishwa Mahakamani 

Kwa upande wake kamanda wa uhifadhi wa  Wanyama Pori kanda ya Kusini Mashariki, Abraham Jullu amewataka wananchi kutoa taarifa kwa taasisi zinazohusika pindi wanapoona Wanyama wameingia kwenye maeneo ya makaazi ya watu

Alisema  baada ya malaka hiyo kuimarisha ulinzi latika maeneo ya hifadhi kwa lengo la  kudhibiti vitendo vya ujangili , hivi sasa majangili hawaingii tena katika maeneo  hayo  ya hifadhi



"Kwa  uzoefi wangu  mara nyingi wanayama wanaouliwa ama kuwindwa na majangili ni wale waliotoka nje ya misiti ama maeneo ya hifadhi za mamlaka hizo na kwenda nje  ya maeneo ya hifadhi , hivyo nitoe Wito kwa wananchi kutoa taarifa jwa mamlaka zinazohusika pindi tu wanapoona wanaya katika maeneo yao ili tuweze kuudhibiti majangili kwa manufaa ya Nchi na Taifa kwa ujumla" alisema  Abraham Jullu 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI