Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo amesema mnamo tarehe 28 mwezi huu huko mlandizi kibaha mkoani Pwani kumetokea ajali ya Magari matatu kugongana na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo mhadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Prosper Ngowi na majeruhi wawili.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha ofisini kwake amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12;20 asubuhi katika maeneo ya miwaleni, halmashauri ya wilaya ya kibaha kwenye gari lenye usajiri wa namba T 608 AGV likiwa na tela lenye namba T 317 AQM aina ya Scania likiendeshwa na Raymond Kimaro (36) mkazi wa Ubungo likitokea nchini Kongo kwenda Dar es salaam.
Alisema Scania hilo lilihama upande wake wa barabara na kugonga gari lenye namba T 256 CMF aina ya Noah lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Morogoro na kusababisha kontena kuchomoka na kuangukia gari SU 38223 aina ya Toyota land cruiser iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kwenda Morogoro ikiendeshwa na Innocent Gerson Mringo na kusababisha vifo vya watu wawili.
Aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na Profesa Prosper Ngowi (55) mchaga na Innocent Gerson (33) mkazi wa Dar es salaam na Dereva na kujeruhi watu wawili ambao ni Raymond KImaro(39) mchaga mkazi wa ubungo na dereva wa T 608 AGV Abdallah Mohamed na Mika (33) mnyaturu mkazi wa Dar es salaam Dereva wa Noah na kusababisha uharibifu wa magari hayo.
Kamanda Lutumo alisema Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa hata hivyo uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya scania kuhama upande wake wa barabara na kugonga gari aina ya noah na kupelekea kontena kuchomoka na kuliangukia gari aina ya Toyota land cruiser.
Mwili wa marehemu Profesa Ngowi umehifadhiwa hospitali ya rufaa Tumbi na mwili wa marehemu Innocent Gerson umehifadhiwa katika kituo cha afya Mlandizi.
Aidha majeruhi wametibiwa na hali zao ni nzuri huku mtuhumiwa akishikiriwa na jeshi la polisi kwa hatua zaidi.
Hatahivyo Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linawataadharisha watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto kuwa makini na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazosababishwa na uzembe.
0 Comments