Header Ads Widget

RUWASA SASA KUNUSURU NDOA LINDI

Hatua ya Sarikali kupitia Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) kumkabidhi Mkandarasi Helem Contruction Company Limited, Mradi wa maji kwa ajili ya kuanza  utekelezaji katika Ukanda wa Navanga  kumetajwa uwenda ikasaidia  kunusuru  kuvunjika kwa ndoa za wakazi wa Kijiji hiko MWANDISHI HADIJA OMARY,MDTV LINDI 

Mradi huo wa ukanda wa Navanga unaotajwa kughalimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.3 unataraji kuwanufaisha jumla ya wakazi  17,015  kutoka vijiji 8 vilivyopo kata ya Kitumbikwela , Navanga, Nachunyu, Sudi na Mnolela umekabidhiwa mbele ya Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari ambae pia ni Mbunge wa jimbo hilo Nape Nnauye

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Nape  licha ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo alimtaka Mkandarasi aliekabidhiwa mradi huo kutekeleza kwa wakati uliopangwa


Nape alisema Mradi huo ambao umeanza rasmi mara tu baada ya kusainiwa kwa mkataba huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi sita

“Nimemueleza Mkandarasi, kama kuna kazi ambayo hatakiwi kuchezea ni kazi ya jimbo la Mtama, ukichezea kazi ya jimboni kwa Nape huo ndio mwisho wa kupata kazi popote tena bora tuambiane mapema kabla mambo hayajahalibika na fitina hiyo sishindwi nitaanzia kwa Rais mpaka Wizarani” alisema Nape

Hata hivyo Nape amewaondoa hofu Wananchi ambao hawajafikiwa na Mradi huo kwa awamu ya kwanza ambapo alisema kuwa baada ya Serikali kuu kutoa kiasi  kikubwa cha fedha  kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo hatua inayofuata ni kwa Halmashauri kumalizia katika maeneo macheche yaliyosalia

“Vijiji vilivyotajwa sio vyote vitamalizika, kwa maana ya kwamba tulivyovitaja vipo ambavyo havijatajwa kwa hivyo kwenye awamu hii ya kwanza havitapata maji kwa awamu hii, lakini ni kazi yangu mimi kwa kushirikiana na madiwani ambapo  kazi ya kwanza ilikuwa ni hii ya Bilioni 4.3 ambapo kwa sisi kama Halmashauri tusingeweza”

“ lakini kuyasogeza kwenye vijiji na vitongoji  vilivyobaki ni kazi ya Halmashauri mimi na madiwani tutatenga fedha tuyavute maji haya ambayo Mama yetu Samia  ametuletea sasa tuyaporomoshe kwenye maeneo mengine ambayo hayakutajwa” alimaliza Nape

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ameeleza namna serikali ilivyojipanga kumaliza tatizo la Maji safi na salama katika halmashauri hiyo ya Mtama ambapo alieleza kuwa kwa kipindi cha miezi sita  halmashauri hiyo imepokie Zaidi ya bilini 10 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maji


Nao baadhi ya Wananchi hao wameeleza changamoto wanazokabilianazo kwa kukosa huduma ya maji karibu na maeneo yao kuwa ni pamoja na Ndoa zao kuwa hatarini kuvunjika kutokana na waume zao kukosa Imani na wake zao pindi wanapokwenda kutafuta maji

“swala la maji katika Kata hii ya Navanga bado ni changamoto kubwa kwani tunalazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji napengine tunapotoka kwenda katika maeneo hayo kwa kuwa tunatumia muda mrefu wanaume wetu wanakosa Imani kuwa uwenda tunatumia mwanya huo kusaliti ndoa zetu’’ alisema  Mazukuni Ally

“Ndio anakwenda kule kutafuta maji lakini wakati mwingine mtu anaweza kuwa anafanya mambo yake mengine maana anatoka alfajili anakuacha mume wake kitandani hata mipango ya kujenga familia hatupangi vizuri wewe unategemea nini? Kwa hivyo kama mradi huu utakamilika sisi tutafurahi sana”  alisema Issa Kitenge

Kwa upande wake kaimu Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mhandisi William Swilla alisema kuwa kukamilika kwa Mradi huo utasaidia Wananchi wa Maeneo hayo kuongeza Chachu ya kufanya shughuli za kimaendeleo badala ya kutafuta maji kama ilivyo sasa

Alisema Wananchi hao kwa kipindi kirefu wamekabiliwa na Changamoto ya Maji Safi na salama ambapo kwa kutambua Changamoto hiyo Serikali kupitia wakala huo ilifanya usanifu wa Mradi huo mwaka 2020 na kukamilika mwaka 2021 ambapo sasa Mkandarasi amekabidhiwa rasmi mradi huo kwa ajili ya kuanza utekelezaji.

“kwasehemu kubwa ya utekelezaji wa Mradi huu kwa wananchi wa Navanga itaongeza Chachu ya maendeleo kwa kuwa sasa hawatatumia tena muda mrefu kutafuta maji na badala yake watatumia muda huo kufanya shughuli za kujiongezea kipato” alisema Swilla

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI