Header Ads Widget

WANAWAKE WA TANZANIA WANATAKIWA KUJIFUNZA KUFUGA SAMAKI .

 




Na Amon Mtega_ Songea .


 DR.Sonnia Musyoka kutoka chuo cha mambo ya Uvuvi Nchi ya Kenya amewataka wakinamama wa Tanzania kutumia fursa ya kujifunza kufuga  Samaki ili waweze kujiongezea vipato kwenye familia zao.


Wito huo ameutoa wakati wakati wakijifunza tabia za viumbe maji hasa Samaki kwenye mafunzo yaliyojumuisha baadhi ya wakufunzi kutoka vyuo vya taasisi za Uvuvi (FETA) ambayo yamefanyika Songea Mkoani Ruvuma.


Dr.Musyoka amesema kuwa kutokana na fursa zilizopo katika Nchi ya Tanzania zinawawezesha wanawake wa kitanzania kujifunza kufuga Samaki na kuachana na tabia ya kuwategemea wanaume pekee ambao muda mwingi wanakuwa hawapo majumbani.




Amesema kuwa katika ya Tanzania kumebarikiwa na Mungu kuwa na Ardhi kubwa ,maji mengi hivyo hakuna sababu ya kushindwa kufuga Samaki hasa kwa wanawake ambao wapo muda mwingi majumbani.


Akizungumzia urahisi wa wanawake kufuga samaki au kuku ni kwamba utengenezaji wa sehemu za kufugia atawaomaba wataamu wanamtengenezea akisha viweka vifaranga basi kazi kubwa ni kulishia jambo ambalo hakuna mwanamke atakayeshindwa.



Kwa upande wake mmoja wa wafugaji wa Samaki ambaye ni mwanamke Deborah Bochelle amesema kuwa yeye toka aanze kufuga samaki wamekuwa wakimletea manufaa makubwa kwa kujipatia kipato ambacho humsaidia kwenye familia yake.


Mfugaji Deborah amewahamasisha na wanawake wengine kujitosa kwenye ufugaji na kuacha tabia ya kuogopa kwa madai kuwa ufugaji ni kazi ngumu Jambo ambalo huwarudisha nyuma kimaendeleo.


Naye Afisa Mfawidhi wa kituo cha ufugaji viumbe maji wakiwemo Samaki katika mabwawa ya Ruhila yaliyopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Emmanuel Maneno amesema kuwa mbengu za samaki zimezalishwa kwa wingi katika kituo hicho hivyo  amewataka wakazi wa Mkoa huo wakiwemo wanawake kutumia fursa ya kwenda kujifunza namna ya ufugaji wa Samaki pamoja na kujipatia mbegu za samaki hao ili waweze kuwa wafugaji bora.




  Maneno amesema kuwa Serikali imeweka vituo hivyo katika maeneo mbalimbali hapa Nchini ili kumfanya Mwananchi aweze kujifunza namna ya kufuga Samaki ili aweze kujiongezea uchumi.


      

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI