Na Arodia Peter
MKURANGA
Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo, Doroth Semu amesema ni wakati sasa wa kulitambua kundi kubwa la wanawake waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi, kwa kuondoa vikwazo na kuendeleza mapambano yao.
Akihutubia wanawake wa chama hicho kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya chama hicho ya Siku wa Wanawake Duniani leo Machi 8, 2022 wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani, Semu
aliwataka wanawake waliopo kwenye siasa na nyadhifa tofauti watoe ushirikiano na kusaidia kuondoa unyanyasaji, ubaguzi, ukandamizaji dhidi yao.
"Sisi tuliopo kwenye siasa na majukwaa mengine ya kitaaluma tuhakikishe vyama vyetu na taasisi zetu vinagusa matamanio, matarajio, malengo, maslahi yao. Tuungane nao kwa kuwashirikisha, kupaza sauti zao kusukuma ajenda zao ambazo ni ustawi wa jamii kwa ujumla," alisema Semu na kuongeza:
Kwa miongo takribani miwili harakati a wanawake zilipamba moto kufikia kupata nafasi kadhaa kwenye nafasi za uongozi, takwimu zinaonyesha pamoja na jitihada hizo bado kuna wanawake tunawaacha nyuma."
Alisema siku hiyo ni muhimu kwa wanawake kutokana na kwamba inatoa fursa ya kuwaimarisha nchini ikiwamo nafasi za uongozi na uwakilishi.
Naye Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo Taifa, Bonifasia Mapunda aliwata wananchi nchini wajitokeze kugombea nafasi zozote zinazojitokeza za kisiasa na kijamii ili kuonyesha uwezo wao.
"Uongozi ni dhamana ya mwanamke na mwanamme, hivyo zitafuteni fursa kwakuwa hamtaletewa kwenye kisahani, governing nafasi zote kwani hizo nafasi nzuri wanaume wanazitaka" alisema Mapunda.
0 Comments