Header Ads Widget

RC LINDI ATAKA WATOTO WA KIKE KUFUNDISHWA KUPIKA

 

Mwandishi wetu, Lindi



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amewataka wazazi kukaa karibu na watoto wao wakike na kuwapa mafundisho mbalimbali ili waweze kuwa mama bora baadae ikiwemo kuwafundisha kupika na kufanya shughuli mbalimbali a nyumbani.


Kauli hiyo ameitoa katika Tamasha la SAUTI YAKO lililofanyika katika Shule ya Sekondari Lucas Malia Girls Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakati wa maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambapo walizungumza na watoot wa kike ili kutoa elimu kwao.


Watoto wa kike ni taifa linalofuata ili kuweza kuwa mama bora wa kesho wanahitaji kuonyewa njia na kutiwa nguvu ili waweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kutokana na umri wao”


Wanawake tunapitia changamoto nyingi kuna wakati natamani kuweka video ili niwaonyeshe changamoto wanazokutana nazo wananawe mambo wanayopitia viunzi vingapi wanaruka hadi wanafikia ndoto zao nadhani ingewasaidia zaidi”


Niwakumbushe tu hakuna mwanaume anaependa mwanafunzi bali anakutamani tu achaneni nao someni kwa bidii ili muweze kufikia ndoto zetu najua mnamipango mingi mna ndoto kubwa ili kuzifanikishwa lazima mkubali kusoma na kuachana na mambo ambayo yanaweza kuwakatisha masomo yenu” alisema Telack


Ni aibu watoto wa kike hawajui kupika hawajui hata kulima bustani kwanini shule hazianzishi bustani kwaajili ya watoto  hawa ili wakajifunza kazi za mikono”


“Wakiwaita waambie niite dada wanaume haawa sio saizi zao nyie mmbebahatika kusoma na kujiunga na maosmo ya sekondani kazi yenu ni moja tu ya kusoma someni kwa bidii wazazi, walimu jamii vinawategemea nataka niwaambie hakuna kinacho shindikana” alihoji Telack


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya  SAUTI YAKO  Devota Ng’itu alisema kuwa tamasha hilo wamelifanya ili kuhaamsisisha watoto wakike kuwa mama bora baade  na mwanamke bora katika familia zao.


“Unajua natamani kupanua wigo kwa kuwafikia hawa watoto wengi zaidi nchini ili kuweza kuwasaidia naamini leo hapa Ruangwa hawa watoot wa kike kuna kitu wamepata kupitia hili tamasha letu ambapo tunaamini kuwa watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao” anasema Ng’tu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI