Na Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
WAFUGAJI wa kuku wametakiwa kutumia chakula sahihi kwa ajili ya mifugo yao ili mfugaji aweze kuinuka kiuchumi na kuendesha maisha yao ya kila siku mfugaji.
Daktari wa kampuni ya uzalishaji wa chakula cha kuku One One Animal Feeds Dk Dioniz Leonard ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya kilimo,ufugaji na uvuvi kanda ya Mashariki.
Dk Dioniz alisema chakula hicho kinamsaidia mfugaji mdogo kuhakikisha anakuwa mfugaji bora na wa kisasa kwani kwa kuanzia na kuku 100 ana uwezo kufikia malengo na tija ina hiyo inamsaidia kuepukana na changamoto za magonjwa.
“Sisi One One tupo kwa ajili ya kumuinua mfugaji wetu na wafugaji kunawatembelea na kumpa elimu ili aweze kumudu ghrama,kuepuka magonjwa ya kuku na yanayosababishwa kufa na kumpa hasara mfugaji,”alisema
Katika maonyesho hayo Meneja wa Azania Benki Morogoro Makalla Mbura akizungumza mara baada ya banda la benki hiyo kutembelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alisema benki hiyo ni ya kizalando imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya kilimo kwa kukopesha wakulima kwenye shughuli za shamba ikiwemo wakulima wa mbogamboga na matunda.
Alisema mkopo wanaotoa hauna ukomo na kwamba kikubwa ni katika kuhakikisha mkulima anafaidika na kuongeza thamani ya kile anacholima.
“Tumekuwa tukikopesha wakulima kwa ajili ya shughuli za shamba lakini pia katika ununuzi wa vifaa na zana za kilimo kama trekta na kwenye mifugo,”alisema meneja huyo.
0 Comments