Header Ads Widget

WANANCHI WA KATA YA BAKOBA WAOMBWA KUTUNZA MITI AINA YA PALM ILI KUPENDEZESHA MAZINGIRA YA KATA YAO.

 


Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.


Wananchi wa kata ya Bakoba halmashauri ya Manispaa ya  Bukoba mkoani Kagera wameombwa kutunza miti maarufu  'PALM TREE' iliyopandwa na baadhi ya viongozi wa mkoa huo Kwa lengo la kupendezesha mji pamoja na kutunza mazingira.


Kauli hiyo umetolewa na diwani wa kata Bakoba Shaban Rashid Katika mkutano wa adhara uliofanyika maeneo ya Buyekera kata ya Bakoba halmashauri ya  manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na taasisi binafsi ambopo baadhi yao walishiriki Katika upandaji wa miti hiyo.


"Miti hii imetolewa na ndugu yetu na mzawa wa kata hii anayeishi nje ya nchi Kwa lengo la kupendezesha mji wetu wa Bukoba na Leo tutapanda miti mitatu maarufu kama 'Palm tree' itapandwa na watu watatu nao ni mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba  Mhe. Gibson Godson, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Eng. Pasaka Bakari pamoja na aliyekuwa mbunge wa Bukoba mjini Kwa tiketi ya CCM mheshimiwa balozi Khamis Sued Kagasheki, miti hii tushirikiane kujitunza vizuri ikawe alama ya viongozi hawa huko mbeleni" amesema diwani Shaban.




Kwa upande wake mmoja wa wana kamati wa mladi wa kuhifadhi mazingira 'Palm tree' Bi. Diyana Deus wakati akizungumza na waandishi wa habari  amesema kuwa, miche hiyo itapandwa katika barabara zote za Manispaa kwa lengo la kuhakikisha Mazingira ya Mji wa Bukoba unapendeza.


" Tunatarajia kupanda Palm tree Katika barabara zote zinazopatikana katika mji wa Bukoba, tumejipanga vyema lengo letu ni  kupendezesha mji wetu,  miti hii ni rafiki Kwa mazingira haina madhara yoyote" amesema Deus. 



Aidha ameziomba taasisi mbalimbali kujitokeza katika kuleta maendeleo kama alivyofanya na kumuunga mkono ndugu Justine Kimodoi ambaye ni mzaliwa wa Bukoba anayeishi Texas Malekani aliye kuja na wazo la kuipendezesha Bukoba kwa kupanda miti ya Palm.


" Miche hii inagharama kubwa, vipo baadhi ya vikundi vinavyojihusisha na uzalishaji wa miche kwa bei elekezi nawashauri  watumie fursa hiyo kuotesha Miche ya miti hiyo kwa wingi ili iweze kuwaingizia kipato"



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI