Header Ads Widget

WANANCHI KATA BAKOBA WARIDHIA ENEO LA SOKO LIBADILISHWE MATUMIZI.

 





Na, Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA. 


Wananchi wa kata ya Bakoba    Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera  wameridhia ombi  la diwani wa kata hiyo mheshimiwa Shaban Rashid la kubadili matumizi ya  soko la nyakanyasi litumike kujenga kituo cha afya kutokana na kuwepo changamoto ya ukosefu wa kituo cha afya katika kata hiyo.


Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa adhara  wa diwani wa kata hiyo uliofanyika Buyekera gengeni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali pamoja na taasisi binafsi ili kuelezea mambo ambayo ameyafanya tangu amechaguliwa kuwa diwani wa kata ya Bakoba na kuelezea mipango aliyonayo ya kimaendeleo ya kuinua kata hiyo.


 “ Nilimfuata mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Bukoba na kumuambia tatizo hili la ukosefu wakituo cha afya katika kata yetu  aliniambia endapo tupata eneo tumjuze tuone namna ya  kuandaa utaratibu , lakini pia mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Steven Byabato aliniambia kuna fedha zaidi ya million 400 kwaajiri ya ujenzi wa kituo cha afya unaeneo? Nikasema subiri ,sasa naomba tukubaliane kwa pamoja eneo la soko ya nyanyasi libadilishwe matumizi kwani nishapokea maoni ya watu wengi wakiomba hivyo kutokana na  uchache wa wafanya biashara wa soko hili na wao tutawapatia eneo jingine kwani sio wengi” amesema Shaban.


Aidha diwani huyo amemuagiza katibu wa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini kumfikishia salamu hizo kwa mbunge wa jimbo hilo Steven Byabato kuwa wananchi wa kata ya Bakoba wamepitisha kubadili eneo la soko la Nyakanyasi litumike katika kungenga kituo cha afya hivyo wanaomba awaunge mkono.





Naye Bi. Zurufa Ally mkazi wa kata ya Bakoba amempongeza diwani wa kata hiyo  pamoja na wananchi wenzake kwa uamzi walioufanya wa kubadili matumizi ya soko Nyakanyasikutumika kujenga kituo cha afya na ameiomba serikali kuwaisha ujenzi wa kituo hicho ili kunusuru uhai wa wananchi wa kata hiyo.


“Tulikuwa kwenye utumwa mkubwa mara uende katika kituo cha afya  Zamzam waseme nenda Buyekera, ukienda Buyekera nao muda mwingine wanafunga mapema kwahiyo sisi kama wananchi tumeridhia eneo hilo libadilishwe matumizi ili tupate sehemu ya kujengewa kituo cha afya ila wito wangu kwa serikali waangalie eneo jingine la kuwaweka wafanya biashara waliopo japokuwa niwachache na  kutu harakishia  ujenzi wa kitu hicho”.



Katika Mkutano huo kumefanyika zoezi la upandaji wa miti aina ya PALM TREE kwa udhanini wa ndugu Jastine Kimodoi, liliofanywa na baadhi ya viongozi akiwemo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini balozi Hamisi Kagasheki na kuwaomba wananchi  kuitunza miti hiyo kwani inaumuhimu mkubwa ikiwemo kupendezesha mjini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI