Header Ads Widget

WANAFUNZI 2,454 WASHINDWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

 


IMEBAINIKA kuwa wanafunzi 2,454 waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu kwenye mtihani wao wa darasa la saba hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa


Kutokana na hali hiyo Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ametaka kutafutwa kwa wanafunzi hao ili wajiunga na masomo yao kabla ya tarehe ya mwisho ya kuripoti Machi 31.


Hayo yamebainika wakati wa kikao cha uongozi wa mkoa na wadau wa elimu ambapo hadi Machi 18 wanafunzi hao walikuwa bado hawajaripoti kwenye shule walizopangiwa.


 Kunenge alisema kuwa  kuna kitu cha kufanya kwani wazazi husika wapo wachukuliwe hatua za kisheria kwani haiwezekani wanafunzi hao wasiripoti ili hali wazazi au walezi wapo lazima

kifanyike kitu ili kupatikana watoto hao na kama wameenda shule binafsi basi ijulikane kwani watoto hao ni wengi sana na hatua za kisheria zichukuliwe.


Kwa upande wake ofisa elimu mkoa wa Pwani Sara Mlaki alisema kuwa kwa mwaka 2021 wanafunzi

waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ni 32,331 wakiwemo wavulana 15,636 na wasichana

16,695 ambapo wote wamechaguliwa kujiungaa na Kidato cha kwanza.

Naye mdau wa elimu Alhaji Yusuph Mfinanga alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya utaulu na kuwena motishakwa walimu na wanafunziwanaofanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI