Header Ads Widget

WAKALA WA MBEGU NCHINI ASA WATAKIWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBEGU BORA

 

 Mtendaji mkuu wa ASA,Dkt Sophia Kashenge akikangua mbegu bora zinazalishwa na wakala

 Na Lucas Raphael Dodoma

 

WAKALA WA MBEGU NCHINI ASA WATAKIWAA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBEGU BORA

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof Siza Tumbo amewataka Wakala wa Mbegu nchini ASA ,kuhakikisha wanatoa elimu ya matumizi bora ya mbegu kwa wanunuzi na wakulima ili kuongeza asilimia ya watumiaji wa mbegu bora

zinazosambazwa na wakala huyo nchini

 

Alitoa Kauli hiyo alipokuwa  akifungua kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wizara ya Kilimo Dodma baina ya Wakala wa mbegu nchini (ASA) na wasambazaji walioingia mkataba wa kusambaza mbegu na wakala huyo,

 

Alisema kwamba Wakala anapaswa kuongeza jitihada katika usambazaji ili kuongeza idadi ya wakulima wanaotumia mbegu bora.

 


Prof Tumbo alisema takribani asilimia 10 ya wakulima wanaotumia mbegu

bora ambazo zimeboreshwa hivyo wasambazaji wa mbegu mnapaswa kuwa

maafisa ugani kuwaelimisha wanunuzi umuhimu wa matumizi ya mbegu

bora,jambo litalaochangia kuongeza uzalishaji wenye tija kwa wakulima

kwa kutumia mbegu bora za mazao.

 

“Ni asilimia chache ya wakulima wanaotumia mbegu bora za wakala wa

uzalishaji mbegu,hivyo mnapaswa kuongeza bidii ya kusambaza mbegu kwa

wakulima pamoja na kuwapa elimu ya kuzitumia,”alisema Naibu Katibu

Mkuu.

 


Alifafanua zaidi ya kuwa idadi ya watumiaji wa mbegu bora

ikiongezeka,basi hata soko litakuwa kubwa kwa wakulima kutokana na

kwamba,wakulima hao watakuwa na uzalishaji wa kutosha katika mashamba

wanayozalisha mbegu hizo.

 

Prof Tumbo akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mazao wenye tija ambao unaleta matokeo chanya,alisema mkulima anatakiwa kuwa na viauatilifu,mbolea,mbegu bora na vitu vingine ambavyo vitamsaidia

mkulima kuboresha shamba lake kabla na baada ya msimu wa mavuno.

 

"mpaka leo hii bado wakulima wanahangaika na uzalishaji wa

mahindi kutokana na kutofuata taratibu za kilimo bora kitendo

kinachochangia kupata tani chache za mahindi kwa heka moja ya

shamba,ukilinganisha na mkulima anayefuata matumizi bora ya kilimo "alisema Prof Tumbo.

 

Alisema,wakulima wakizingatia kufuata kanuni bora za kilimo,watasaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa uzalishaji wa mbegu bora ambazo zitaleta tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

 

Alisema serikali kila wakati  wanasisitiza suala la matumizi ya mbegu bora ,Viuatilifu zana za kilimo kwa sababu vitu hivyo ukiwa navyo na wakijua kuvitumia vizuri wanaweza kupata mazao yale ambayo tunasema wanazalisha kwa tija.

 

Naye Mtendaji mkuu wa ASA,Dkt Sophia Kashenge alisema maelekezo waliopewa na Wizara watayafanyia kazi kikamilifu ikiwemo kuhimiza wadau

wasambazaji wa mbegu katika maeneo ya pembezoni kuongeza bidii ya

kuwafikishia wakulima kwa wakati wote hasa msimu wa Kilimo

 

Alisema moja ya changamoto ambayo inawasumbua wakulima ni

ucheleweshaji wa mbegu,hivyo hilo watalifanyia kazi ili kuhakikisha

wanaboresha hilo,ambalo anaamini litasaidia kutatua changamoto .

 

Hata hivyo alisema kikao hicho na wadau wasambazaji wa mbegu ambao

wameingia mkataba wa kusambaza mbegu kwa wakulima,kitasaidia

kuimarisha Ushirikiano baina yao,kutokana na kwamba sasa hivi serikali

imeelekeza nguvu katika kufanya kazi na sekta binafsi.

 

“Tunaishkuru serikali kwa kuamua kufanya kazi kwa karibu na sekta

binafsi,hili litaongeza ufanisi katika usambazaji wa mbegu,”alisema Dkt

Kashenge.

 

Alisema wanapofanya kazi pamoja na sekta binafsi,wanaongeza wigo wa

utendaji,ambapi  kiu yao ni kuhakikisha usambazji wa mbegu

unaongezeka kwa kiasi kikubwa ili mkulima asipate tabu ya kupata

mbegu,pindi msimu wa kilimo unapowadia.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI