Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina leo tarehe 28, Machi, 2022 anaungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha Gwiji wa Uchumi Tanzania na aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam, Marehemu Prof. Honest Prosper Ngowi aliyefariki kwa ajali ya gari leo.
Mhe. Mpina amesema amepoteza Kaka na Mwalimu wake wa Uchumi, Taifa limepata pigo na pengo kubwa kupoteza rasilimali adimu Profesa Honest Prosper Ngowi.
Mhe. Mpina anakumbuka alipomtembelea Prof. Ngowi kwa mara ya mwisho ofisini kwake Dar es Salaam, Februari 24, 2022 ikiwa ni mwezi mmoja tu uliopita, Prof. Ngowi pamoja na kumkabidhi zawadi ya vitabu mbalimbali vya uchumi alivyoviandika enzi za uhai wake lakini pia alitumia nafasi hiyo kumshauri na kumtia moyo Mhe. Mpina kukamilisha vyema safari yake ya masomo ya Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Fedha (PhD in Finance) anayoendelea nayo, namna ya kuwa mwakilishi bora wa Wananchi wa Jimbo la Kisesa na kulitumikia taifa kikamilifu.
0 Comments