Na Amon Mtega,_Mbinga.
WADAU wa kuhudumia wageni (Watalii) katika Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wametakiwa kutumia ya vivutio vilivyopo Wilayani humo ikiwemo milima ili kuongeza idadi ya Watalii Wilayani humo.
Wito huo umetolewa na Afisa Utalii nyanda za juu kusini katika Wizara ya Maliasili na Utalii Sixtus Malangalila wakati wakitoa mafunzo ya Uviko 19 kwa wadau wa Wilaya ya Mbinga wanao hudumia wageni pindi wanapotalii kwenye vivutio mbalimbali vya vilivyopo Wilayani humo.
Malangalila akizungumza kwenye mafunzo hayo ambayo yamekuwa na washiriki zaidi 150 yaliyofanyika siku mbili amesema kuwa Wilaya ya Mbinga inaonekana kuwa na vivutio vingi ikiwemo vivutio vya milima ,hivyo ikitangazwa kikamilifu itakuwa na fursa kwa wadau hao pamoja na wakazi wa Wilaya hiyo kwakuwa vivutio hivyo vitawaongezea mapato.
Afisa huyo amesema kuwa baadhi yao hasa wadau wa ukanda huu wamezoea kuwa vivutio ni ziwa Nyasa tu ,kumbe hata milima iliyopo inakuwa ni moja ya vivutio ambavyo vinaweza kuongeza mapato na mwisho wa siku Serikali inanufaika na wadau pia.
Kwa upande wake mgeni rasmi Stuart Kuziwa ambaye ni kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga mji wakati akifunga mafunzo hayo amewataka washiriki waliopatiwa mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi yaweze kuleta tija ndani ya Wilaya hiyo pindi wanapo wahudumia wageni.
Naye Amanyisye Ngonepo diwani wa kata ya Bethrehemu ambaye ameshiriki mafunzo hayo na kupatiwa cheti amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoifanya ya katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya Utalii.
Hata hivyo Ngonepo ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii inayoongonzwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea mjini kwa kusimamia mafunzo hayo pamoja na kuimarisha sekta hiyo hasa katika uibuaji wa vivutio mbalimbali vya Utalii.
Pia mshiriki Veronica Nkondola amesema kuwa mafunzo hayo ya Uviko 19 yatawasaidia pindi wanapotoa huduma kwa wageni namna ya kuweza kujikinga na kuwakinga wageni wasipatwe na madhara mbalimbali ya kiafya.
0 Comments