kaimu mkurugenzi wa kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC) Anna Lyimo
Na Fatma Ally MDTV ,DAR
Imeelezwa kuwa kutokana na milango ya uchumi kufunguliwa nchini Tanzania, katika awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kumekuwa na mwamko mkubwa wa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC) Anna Lyimo wakati alipokua katika Mkutano wa wadau wa uwekezaji kutoka nchini Qatari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Lyimo amesema kuwa kituo hicho, leo kimepokea wawekezaji 25 kutoka nchini Qatari kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini.
Amesema kuwa, wawekezaji hao wamelenga kuwekeza katika Sekta ya mifugo, uzalishaji wa vifaa tibaa, madawa, Utalii, Usafiri wa Anga pamoja na Uchumi wa Blue.
Ameongeza kuwa, lengo la TIC kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ni kupeana taarifa muhimu katika Sekta walizochagua wawekezaji hao kupitia fursa zilizopo nchini.
Hata hivyo, amesema kuwa wawekezaji hao pia watatembelea Zanzibar na kupokelewa na kituo Cha uwekezaji Cha Zanzibar Ili kuangalia fursa zizopo ambapo wanatarajiwa kuondoka nchini tarehe 29.
Hata hivyo, ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani kwenda kutembea vituo vya kanda na tovuti ya kituo hicho kupata taarifa, ili waweza kujua wageni gani wamefika na wanataka kuwekeza katika maeneo gani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Ranchi ya Taifa Dkt. Peter Msophe amesema kuwa wapo tayari kufanya uwekezaji wa pamoja na wawekezaji wa nchini Qatari, huku akikishukuru kituo cha uwekezaji kwa kuwainganisha na wawekezaji.
Amesema kuwa, kampuni ya Ranchi ya Taifa inashughulika na uzalishaji, uchakataji na uuza wa mazao ya mifugo hasa upande wa nyama, mbuzi, Ng'ombe na kondoo na bidhaa za ziada kama majani na mbolea.
Aidha, amesema kuwa, kutokana na ziara waliofanya kwenye maonesho ya kilimo yakifanyika nchini Qatar yamezaa matunda ambapo leo wawekezaji wa nchini Qatar wamefika Tanzania kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na kuangalia fursa zilizopo.
"Wiki mbili zilizopita tulienda kuiwakilisha Serikali yetu katika maonesho makubwa ya tisa ya kilimo na Mazingira yaliyofanyika Doha nchini Qatar, ambapo ndio leo ziara ile imezaa matunda hayo"amesema Dr Msophe.
0 Comments