Hamida Ramadhan Dodoma
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imewakutanisha Asasi za Kiraia takribani 25 kutoka mikoa 13 Tanzania bara na 1 Zanzibar asasi hizo ni zile zinazotekeleza mradi unaofadhiliwa na foundation for civil society kwa ajili ya kukomesha ukatili wa kijinsia hapa nchini.
Akiongea na waandishi wa Habari Afisa habari kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Jackson Malangalila amesema lengo ni kungalia robo ya pili ya utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia na ni kwa namna gani mradi umeweza kufanikiwa na changamoto nizipi zilizojitokeza huku wakishirikishana kwa pamoja kujifunza mbinu za utekelezaji wa mradi huo ili kufikia malengo ya kuhakikisha wanaondoa ukatili wa kijinsia hapa nchini.
"Kama taifa tunatekeleza Mpango wa Taifa wa kukomesha Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto Hivyo basi tumekutanisha wadau hawa wanaotekeleza mradi wa kutokomeza ukatili ili kwa pamoja waone jitihada zao na kwa ummoja wao kuweza kujipanga zaidi katika kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomezwa hapa nchini,"
Na kuongezeka kuwa "Wadau wamekutana hapa lengo ni kusikia kutoka kwao na kutoa taarifa juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza mradi huu lakini pia kuona changamoto na jinsi gani tunaweza kusonga mbele kwani changomoto zilizopo Simiyu zinaweza kuwa tofauti na Arusha au Zanzibar na ndio maana tumewakutanisha hapa Dodoma kubadikishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kukomesha ukatili" amesema Malangalila.
Kwa upande wake Immaculate Komba afisa Mradi wa kupiga ukatili Kutoka shirika TVMC amesema mradi huo wanatekekeza katika mkoa wa shinyanga na katika kata saba nawamechukuwa shule za sekondari 4 na primary 4 ambapo wanawajengea uwezo kamati za kutokomeza ukatili zilizopo ngazi za kata na wanafunzi ambao ndio wahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili.
Amesema wamekuwa wakizijengea uwezo kamati za kutokomeza ukatili zilizopo chini ni kwajinsi gani wanaweza kujikinga pale wanapopamba na kesi za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo mafanikio yaliopatikana nipamoja na kuweza kuelimisha jamii ni jinsi gani wanaweza kutoa taarifa pale wanapoona kuna vitendo vya kikatili vinapofanyika kwa watoto na wanawake ambapo kupitia kamati hizo matukio 19 yameripotiwa katika kata 17 za mradi.
Naye Paul Kigeja anafanya kazi na shirika la SPRF wanapatika mkoa wa Singida wilaya ya Ikungi wakitekekeza mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wakiangazia hasa masuala ya ukeketaji kwa wanawake mimba na ndoa katimia umri mdogo vipigo ubakaji ulawiti kusafirisha watoto kutoka Singida kwenda kufanya kazi za ndani katika mikoa ya kimkakati amesema katika utekelezaji wao hali imebadilika tofauti na kipindi walivyoanza matukio ya kikatili yamepungua ukilinganisha na mwanzo lakini changamoto bado zipo licha ya kupiga hatua na zinarudisha nyuma harakati hizi za kuwatetea wanawake na watoto.
Amesema changamoto kubwa katika mkoa wa Singida ni mashauri kuishia ngazi ya familia hali iliyokuwa kama tabia kutokana sehemu kubwa wananchi wanaoishi kule ni ndugu hivyo zikitokea kesi kama hizo wamekuwa wakiitana na kuchinja mbuzi au kutoa pesa kesi hile inaishi kimyakimya .
"Wenyewe wanaiita NJUGUDA utakuta ni kesi ya jinai suala la ubakaji mimba na ndoa katika umri mdogoimetokea sehemu fulani lakini wanamaliza kifamilia ," amesema .
Naye Tatu Mrutu anafanya kazi na shirika la Action for Justice in Sociaty (AJISO) kilimanjaro ametoa wito kwa kamati katika kata na Halmashauri husika zinatakiwa kuwa kipaumble kuhakisha ukatili na taarifa zote za ukatili zinazofika kwao wanazifanyia kazi kwa haraka na zinatoa matokeo mazuri kwa wahanga wa vitendo hivyo vya ukatili.
"Naomba nitoe rai kwa Wajumbe wa kamati wasiwe miongoni mwa wanao sababisa vitendo vya ukatili kwani Kuna kesi moja imetokea polisi kata alibaka mtoto wakati inafahamika wazi polisi kata ni mjumbe wa kamati za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hali inayotupa wakati mgumu na jamii kuogopa kutoa taarifa kama wajumbe wakamati ndio wanafanya vitendo hivyo vya kikatili," amesema
0 Comments