Na,Jusline Marco:Arusha
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru imekabidhi miongozo ya TAKUSKA ya kupambana na rushwa nchini kwa kushirikisha vijana wa SKAUTI inayolenga kutoa mafunzo kwa vijana mashuleni.
Akikabidhi miongozo hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Arumeru ,Deo Mtui amesema serikali katika mapambano dhidi ya rushwa imeamua kuwaandaa vijana wakiwa bado wadogo.
Mtui amesema lengo la TAKUKURU kuungana na SKAUTI kutengeneza TAKUSKA ni ili kuhakikisha vijana wanakuwa wazalendo,waadilifu,waaminifu pamoja na wawajibikaji katika Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango ameipongeza TAKUKURU NA SKAUTI kwa kuanzisha mkakati huo na kuzishauri Idara ya Elimu Sekondari na Elimu Msingi katika halmashauri zote mbili za Wilaya hiyo kutafuta ofisi katika majengo ya serikali kwa ajili ya SKAUTI.
Kwa upande wake Kamishna wa SKAUTI Wilayani humo,Justice Yona ametoa rai kwa viongozi,wakuu wa Idara ya sekondari na msingi wa halmashauri hizo kuona umuhimu wa kuandaa kikoa kitakachotoa elimu kwa wataalam ili kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa miongozi hiyo.
0 Comments