Header Ads Widget

SPIKA DKT TULIA AWASILI NCHINI INDONESIA





SPIKA  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Tulia Ackson (Mb), amewasili Bali nchini Indonesia leo Machi 21, 2022 ambapo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia,  Dkt. Ramadhani Dau katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ngurah Rai.


Wakati huo huo, Dkt.Tulia amehudhuria kikao cha kwanza cha mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na kusikiliza mawasilisho ya Maspika washiriki juu ya dhima inayohusu uhamasishaji wa Mabunge katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha Dkt.Tulia anatarajia kulihutubia Bunge la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kesho tarehe 22 Machi, 2022 saa 4 asubuhi katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI