Header Ads Widget

SERIKALI YABAINI TOVUTI FEKI INAYOFANYA UTAPELI WA AJIRA

 


Na Hamida Ramadhan,MDTV  Dodoma

MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa amesema kumeibuka tovuti iliyotambulika kwa jina la www.Sensatanzania.com ambayo imekuwa ikitangaza kuwepo kwa nafasi za kazi za makarani wa Sensa na tayari baadhi ya Watu wameshajisajili kwenye Mfumo huo wa malipo na Kusema hao ni matapeli.


Amesema NBS na OCGS inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa Serikali haijaanzisha tovuti rasmi ya Sensa hivyo tovuti hiyo sio na haitambuliki na Serikali


Akiongea lea tarehe 28 Machi 2022 na waandishi wa habari Mtakwimu huyo amesema nafasi za Ukarani na usimamizi wa Sensa bado hazijatangazwa na muda ukifika zitatangazwa rasim kupitia tovuti na mitanda ya kijamii ya NBS na OCGS,pamoja na Redio,runinga na magazeti Mara baada ya taratibu zote za Serikali zitakapokamilika.


Aidha amesema kazi ya kuwapata hao wa Sensa itasimamiwa na Kamati za Sensa za mkoa ambazo wenyeviti wake ni wakuu wa mikoa husika ambapo ameeleza nia ya Serikali kufanya hivyo ni kuhakikisha Watu wote wanaotaka kufanya kazi za Ukarani na usimamizi wa Sensa watoke katika maeneo yao wanayoishi 


"Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar OCGS inapenda kutoa tahathali kwa wananchi wote kuwa hadi Sasa haijatangaza nafasi za kazi za makarani wa Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022,"amesema Mtakwimu huyo.


Hata hivyo amewataka watanzania  wote wenye nia ya kuomba nafasi hizo wafuatilie rasimi ya Serikali  ikiwemo tovuti za Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar OCGS na Ofisi zawakuu wa Mikoa na Wilaya ,Kata naTarafa


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI