MKOA wa Pwani umeanza oparesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu waliyoingia kinyume cha sheria mkoani humo.
Akizungumza na maofisa Uhamiaji na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa zoezi hilo litadumu hadi Machi 23.
Kunenge alisema kuwa zoezi hilo ltazingatia sheria utaratibu na kanuni katika kuwakamata wahamiaji haramu ambao wameingia nchini bila kufuata utaratibu.
"Lengo la oparesheni hii ni kuchunguza ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaoishi nchini kinyume cha sheria ili kuhakikisha nchi inabaki salama kwani baadhi yao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kihalifu,"alisema Kunenge.
Awali Ofisa Uhamiaji mkoa wa Pwani Omary Hassan alisema kuwa kuwasaka wahamiaji haramu na kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
Hassan alisema kuwa wahamiaji hao wanapobainika itawanyima fursa kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine ambapo katika operesheni hiyo ya zaidi ya wiki moja ni maalumu inatokana na agizo la Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Anna Makakala ameagiza kufanyika ili kuwakamata wahamiaji haramu.
Aliongeza kuwa baadhi ya raia wa nje wanaingia kihalali lakini vibali vinapoisha hawakati vingine ili viwaruhusu kuendelea kuishi nchini lakini wale wanaotoka pembe ya Afrika wengi wanafanya hapa kama njia ya kupita kuelekea Kusini mwa Afrika hasa wale wanaotoka Ethiopia ambapo kwa sasa wimbi la wahamiaji haramu kwa sasa limepungua.
0 Comments