Na Chausiku said _Mwanza.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Marry Massanja amewataka wakala wa huduma za misitu nchini (TFS) kubaini maeneo ambayo yatakuwa sahihi katika upandaji miti yatayosaidia kuwa na upandaji miti wenye tija.
Ameeleza hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa na siku ya misitu Duniani kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya sabasaba wilayani Magu Mkoani mwanza.
Marry ameeleza kuwa kutokana na changamoto za uharibifu wa misitu kumepelekea upungufu wa Kukosekana kwa kuni, mkaa pamoja na mbao za kujengea.
"Wilaya ya Magu ni wilaya moja wapo zinazokabiliwa na ukame kutokana na ukataji miti wa holela usio na mpangilio mzuri" Alisema Marry.
Ameeleza kuwa kutokana na kasi ya uhalibifu wa maeneo ya hifadhi ya misitu unaotokana na uvunjaji wa mazao kiholela na ukataji miti ovyo bidhaa hizo zimekuwa adimu wakati mwingine zinapatikana kwa bei ghali.
Aidha amefafanua kuwa kumekuwepo na dalili za hatari za upotevu wa mvua za kutosha na kuwepo kwa mvua zisizoeleweka pamoja na kukauka kwa vyanzo vya maji vinavyotegemewa.
"Miti mingi imekata na hakuna hatua yeyote ambayo imewahi kuchukuliwa ya kurudisha miti mingine na hali inazidi kuwa mbaya karibu wilaya zote za kanda ya ziwa" Alisema Marry.
Maadhimisho yawe chachu ya kupanda miti katika maeneo yetu tunayoishi na shughuli hiyo ya upandaji miti hazitofautiani na shughuli nyingine za kilimo cha mazao ya chakula.
Ametoa wito kwa wizara ya maliasili kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa upandaji miti na uhifadhi wa misitu na kutambua faida za maliasili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Magu Salum kalli ambaye amemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Robert Gablier ameeleza kuwa mkoa umeadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti mil 3237871 na zoezi hilo litakuwa endelevu.
" kama tunavyofahamu miti ni uhai, miti huleta uoto wa asili na kuleta hali ya hewa yenye mvuto" Alisema Kalli.
Mkurugenzi wa misitu na nyuki Ezekiel Mwakalukwa ameeleza kuwa lengo la kuanzisha maadhimisho hayo ni kutoa elimu nakuelimisha watu wote juu ya umuhimu wa aina zote za misitu hapa duniani.
0 Comments