Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE KUTOA HATI ZAIDI YA 300 CHALINZE

 





-Atoa onyo kwa wavamizi wa maeno


Na Andrew Chale, Chalinze.


Mbunge Jimbo la Chalinze  ambaye pia Naibu Waziri wa Ardh, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Machi 7,2022 anatarajiwa kugawa hati zaidi ya 300 tukio litakalofanyika Halmashauri ya Chahalinze Mkoani hapa.


Hayo ameeleza jana Machi 6 katika kijiji cha Diozile kilichopo Kata ya Msoga wakati wa kuhitimisha ziara yake ya Kata Nne za baadhi ya Jimbo hilo.


 Awali akiwa katika mkutano huo, ametoa agizo nchi nzima kwa wavamizi wa maeneo bila kufuata sheria na taratibu kwa kueleza kwamba suala hilo ni uvunjifu wa sheria na ni lazima likome mara moja. 


Ambapo ametoa agizo hilo katika kijiji hicho cha Kidozile kufuatia mgogoro na tatizo kubwa la uvamizi wa maeneo na kufanya shughuli za uchomaji wa mkaa na kilimo kinyume na sheria.




"Hakuna nafasi kwa Watu kwenye nchi yetu kuvamia maeneo bila kufuata sheria. Kumekuwa na watu wanaojulikana kama tegesha ambao wamekuwa wakivamia maeneo na kujitegesha ili baadae waonewe huruma na Serikali ili wapewe maeneo hayo. Jambo hili halikubariki." Alisema Mhe. Ridhiwani.


"Natoa agizo kwa nchi nzima kwamba hakuna nafasi ya kuingia na kuishi sehemu bila kufuata utaratibu. 



Watu wanaofanya hivi ni wahalifu kama wahalifu wengine. Utaratibu upo wazi kwa mtu anayetaka kuingia na kuishi sehemu ni lazima afuate sheria kwa kujitambulisha kwa Kijiji husika au Serikali ya eneo analotaka kuishi kwasababu Serikali yetu haikatazi mtu yeyote kuishi popote lakini lazima afuate sheria." Alisema Mhe. Ridhiwani.


Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema lazima tumalize migogoro ya ardhi na kudhibiti uvamizi wa maeneo kwasababu nchi haiwezi kuendeshwa kwa watu kuvamia vamia tu maeneo bila kufuata sheria na kuwa na migogoro ya ardhi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI