Header Ads Widget

MJUMBE WA CWT TAIFA AWAOMBA WALIMU SONGEA DC KUFANYA KAZI KWA BIDII .

 



Na Amon Mtega, Songea.



MJUMBE wa kamati tendaji Taifa wa Chama Cha Walimu (CWT) Sabina Lipukila amewaomba Walimu wa Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma kufanya kazi ya kuwafundisha wanafunzi kwa bidii na kuzingatia weledi ili mwaajili aendelee kuwa na kuwa na moyo wakutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika mazingira ya kazi.

  

 Lipukila ameutoa wito huo wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kuinua Taaluma kwenye shule za Msingi na Sekondari zilizopo kwenye Halmashauri ya Songea Vijijini  kutokana na shule hizo kwa miaka kadhaa licha ya ufikia malengo bado hali ya taaluma imekuwa hairidhishi.


 Mjumbe huyo mesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan umejitahidi kuweka miundombinu mbalimbali ikiwemo ya Elimu hivyo ni vema Walimu wakatumia fursa hiyo kujituma katika utendaji kazi ili mwisho wa siku taaluma ipande na mwajili azidi kuwatengenezea mazingira mazuri zaidi.



Aidha mjumbe huyo amesema kuwa inasikitisha kusikia baadhi ya Walimu wamekuwa wakifanya mahusiano yasiyo mema  na wanafunzi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi na imekuwa ikiwafanya baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao.


 Hata hivyo Lipukila licha ya kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan pia amempongeza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Wilbert Ibuge ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo kwa kuisimamia kikamilifu Elimu Mkoani humo.


Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe amesema kuwa uzinduzi wa mkakati huo umefikia baada ya kutambua kuwa kwa miaka kadhaa ya nyuma Halmashauri hiyo haikufanya vizuri kwenye upende wa taaluma .


  Mkurugenzi Maghembe akitoa taarifa hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Wilbert Ibuge amesema kuwa mkakati huo utaisaidia jamii wakiwemo na wadau mbalimbali wa Elimu kufanya msukumo wa kutambua changamoto ambazo hujitokeza kwenye sekta hiyo ya Elimu.

  

 Maghembe amesema Halmashauri hiyo ina shule za Msingi 81 kati ya hizo shule 78 ni za Serikali na 03 ni shule zisizomilikiwa na Serikali huku shule za Sekondari zipo 22 kati ya hizo shule 17 ni za  Serikali na shule 05 za binafsi.



 Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mkakati huo aliipongeza Halmashauri hiyo kwa kubuni mkakati huo ambao utasaidia wanafunzi kuwa na ufaulu mzuri.


Mkuu huyo ambaye amemuwakilisha Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais utumishi na Utawala bora amesema kuwa kama mkakati huo utazingatiwa kikamilifu Halmashauri hiyo itegemee kuwa na mabadiliko ya makubwa katika nyanja ya Elimu.

 

 Aidha Ibuge licha ya kupongeza mkakati huo lakini bado ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kusimamia vema miradi ya  ujenzi wa madarasa yatokanayo na Uviko 19 ambayo sasa yanatumika na wanafunzi hao.



 Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mennas Komba akitoa neno la shukurani kwa wadau mbalimbali wa Elimu alisema kuwa maagizo yote ambayo yamependekezwa kwenye mkakati huo kuwa yatafanyiwa kazi.


Katika uzinduzi wa mkakati huo ambao uliyoambana na kaulimbiu ya Elimu bora inawezekana timiza wajibu wako ,huku shule zilizofanya vizuri kwenye taaluma zilipatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na vyeti.

       





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI