Una maoni gani baada ya BASATA kumpiga Stopi Steve Nyerere kuwa msemaji wa shirikisho la Muziki Tanzania unafikiri uamuzi wa kusimamishwa ni sawa au akina Mwana FA wanamuonea donge Kwa kumpa msaa 48 kujiuzulu .
Binafsi nachelewa kusema kuwa shida haupo Kwa Steven Nyerere ila naona tatizo kubwa Kwa Baraza la Sanaa Tazania (BASATA) Kwa kushindwa kufanya kazi Kwa weledi tena pasipo ushirikishaji wa wale wanaowaongoza .
Ni wazi kabisa BASATA inashughulika na Sanaa ila ilipaswa kujua nani anafiti kuwa kiunganishi Cha makundi yote ama kuwa na msemaji wa wanamuziki anayejua Muziki na msemaji wa Wasanii anayejua Sanaa kama Steven Nyerere .
Lakini naamini kupitia makosa haya BASATA wamejifunza jambo kwa wakati mwingine watakuwa makini kuteua mlengwa hasa ili kukuza tasnia husika Kwa kuwa na msemaji anayejua sekta husika .
Hivi leo tuna wanamuziki wakubwa kama Diamond,Alli Kiba na wenzake pia wakongwe kama Chid Benzi ,Fid Q ,Wakazi , Mike T na wengine wengi wote hawa wameshindwa kuwaona hadi kumchukua mchekeshaji kwenda kuchekesha wanamuziki .
BASATA Muziki wa Tanzania si vichekesho watu wanahitaji mtu anayejua Muziki ili asimame kuwasemea wanamuziki sio kuwachekesha japo Muziki ni sehemu ya utamaduni ila Steve Nyerere abaki Bongo Movie .
Naamini kabisa huwezi kukisemea kitu ambacho hukifanyi ni sawa na kuwa msemaji wa wenye Nyumba wakati wewe ni mpangaji hivi BASATA mlitumwa na nani kumteua Steven Nyerere na nani kawatuma kumsimamisha? BASATA Zamu yenu kujiuzulu Kwa mkanganyiko huu mkubwa Kwa Taifa maana hofu yangu BASATA wenyewe hawajui majukumu yao.
0 Comments