Header Ads Widget

KIJANA ALIYENUSURIKA KIFO KWA MANYANYASO,ASHUKURU MRADI WA YAM

 


KIJANA Anord Patrick Kalinga (21) mkazi Mlevelwa kata ya Mdabulo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambae ni miongoni mwa vijana 100 toka kwenye familia duni walioibuliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi  na  mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) amepongeza mradi huo Kwa kumuona NA  FRANCIS GODWIN MATUKIO DAIMA MEDIA


Anord alisema akiwa mdogo alipitia mazingira hatari na hata wakati mwingine alinusurika kifo kutokana na kazi ngumu za mateso alizokuwa akipewa na ndugu zake.



Akitoa shuhuda zake leo kwenye warsha ya Afya ya akili inayoendelea Katika Ukumbi wa Yatima Igoda wilaya Mufindi ,alisema kuwa Kwa upande wake alikuwa amekata tamaa ya maisha hasa kutokana na mazingira magumu aliyopitia .



Hivyo kupitia mradi huo wa YAM anaamini atasimama tena na kupambana kuwa na maisha bora kwani Kwa muda wa mafunzo aliyopata Kuna mambo mengi na mazuri amejifunza ambayo kwake ni kama mtaji .


"Kutokana na changamoto za maisha niliyopitia leo nimenifunza mambo mengi ya kunifanya kusonga mbele kimaisha na Sasa sijuti tena kuwa kijana toka mazingira magumu ila naitumia fursa hii niliyofikiwa kusonga mbele"alisema Anord 


Kuwa  malengo yake ni kwenda chuo cha ufundi Kusoma ufundi magari na udereva ili kupitia kazi hiyo aweze kusimama kiuchumi .


Alisema mbali ya kuwa na maisha duni ili amekuwa nguzo ya familia Kwa kutafuta fedha za kusaidia kuendesha familia yake na kupitia elimu ya ufundi atakayoipata ataweza kuondoa hofu ya kiuchumi inayomkabili Kwa Sasa.



Mkufunzi wa mafunzo haya Dr Heriel Mfangano aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuitumia elimu hiyo kama plani B ya kuendelea na ndoto zao za kumiliki uchumi wao .


Alisema elimu ya ujasiliamali ni nguzo sahihi Kwa vijana hao kuja kukuza uchumi wao na kuondokana na hali ya kujitenga na kuona hawana uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi .


  Halmashauri ya Mufindi chini ya mradi wa FCWC na YAM kupitia ufadhili wa Finland utakelekelezwa kwenye kata za Luhunga ,Ihanu na Mdabulo ni mradi wa miaka minne ulioanza mwaka jana na Utekelezaji wake utakaonufaisha  vijana na  watoto  wanaotoka  katika  familia duni zaidi ya   vijana 770  atika  vijiji 16.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI