Header Ads Widget

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA ARDHI BUNDA MKOANI MARA

 


Na Mwandishi Wetu, Bunda.


KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa Kupanga, Kupima na Kurasimisha unaoendelea Wilayani Bunda Mkoani Mara.



Hayo yamebainishwa na Kamati hiyo ya Bunge ilipotembelea eneo la mradi huo kujionea hali halisi ambapo pia mbali na kuridhishwa, walitoa mapendekezo namna ya uboreshaji zaidi.




Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye aliambatana na Wajumbe wa Kamati hiyo, alibainisha kuwa, Mradi huo umetekelezwa ikiwa ni sehemu ya fedha Bilioni 50 zilizotengwa na Serikali kwenda Halmashauri 55, Bunda ikiwemo. 



Aidha, Kamati hiyo pia ilitembelea mradi wa matofali wa Halmashauri ya Mji-Bunda ambapo wanatengeneza Bikoni za utambuzi wa Ardhi. 


.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI