Header Ads Widget

BMT YAWATAKA WAAMUZI NA WALIMU WA NETIBOLI KUIBUA VIPAJI

 


BARAZA la Michezo Tanzania (BMT) limewataka Waamuzi na Walimu wa Netiboli  kuibua vipaji vya vijana kwenye mchezo huo.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku nane kwa waamuzi na walimu wa mchezo huo hapa nchini  Gerald Mwarekwa kutoka (BMT) amesema mafunzo hayo yawe chachu ya kuhamasisha vijana


Mwarekwa amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuongeza vipaji pia kuendana na dunia inavyotaka na kukabiliana na moja ya changamoto ya waamuzi na walimu.


"Haya ni mafunzo mazuri sana hapa wanatoka na ujuzi na maarifa na muende na kuwasaidia vijana ili matunda yaonekana na mafunzo yalete tija kwani mmeiva nendeni huko hata vijijini,"alisema Mwarekwa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Netiboli (CHANETA) Taifa Devotha Marwa amesema mafunzo hayo yatasaidia kuleta chachu ya mchezo huo na wataibua na kuendeleza vijana.


Naye ofisa michezo mkoa wa Pwani Grace Bureta amesema mafunzo hayo wanapaswa kuyafanyia kazi ili kuwapatia ujuzi wanamichezo ambapo kwenye michezo ya Umitashumta na Umiseta kutakuwa na vitu vya tofauti.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI