Header Ads Widget

BIDEN ASEMA PUTIN NI "MHALIFU WA KIVITA"

   

 

  Rais wa Marekani Joe Biden amemtaja mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kuwa "mhalifu wa kivita" katika hatua ambayo huenda ikazidisha mvutano wa kidiplomasia.

Bw Biden alitoa maelezo hayo akijibu swali la mwandishi wa habari katika Ikulu ya White House.

Hii ni mara ya kwanza kwa Biden kutumia lugha ya aina hiyo kumshutumu Rais Putin, na Ikulu ya White House baadaye ilisema "ni kauli aliyotoa moyoni mwake".

Kremlin, hata hivyo, ilisema ni "maneno yasiyosameheka". "Tunaamini matamshi kama haya dhidi ya mkuu wa nchi hayakubaliki na hayawezi kusamehewa," msemaji wa Dmitry Peskov aliambia shirika la habari la serikali ya Urusi Tass.

Bwana Biden alitoa tamko hilo siku ya Jumatano mjini Washington wakati mwandishi wa habari alipomuuliza rais wa Marekani: "Mheshimiwa Rais, baada ya kila kitu tulichoona, uko tayari kumwita Putin mhalifu wa kivita?"

Rais alijibu "hapana" kabla ya kuulizwa tena swali hilo, na ndipo akabadilisha jibu lake: "Je, umeniuliza kama ningesema ....? ah, nadhani yeye ni mhalifu wa kivita."

Chapisho kwenye akaunti rasmi ya Twitter ya Rais linasema: "Putin ameifanyia Ukraine uharibifu wa kutisha na wa kusikitisha - kulipua majengo ya ghorofa na wodi za kina mama kujifungulia. Huo ni ukatili. Ni ghadhabu ya ulimwengu."

Msemaji wa Habari wa Ikulu ya White House Jen Psaki baadaye alisema rais alikuwa akizungumza kutoka moyoni mwake baada ya kuona picha "za kikatili" za ghasia nchini Ukraine, badala ya kutoa tamko lolote rasmi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS