Adeladius Makwega-DODOMA
Watanzania wametakiwa kuyaombea mataifa ya Ukraine na Urusi kwa kuwa hivi sasa yapo vitani, kwani chokochoko za upande mmoja zinaweza kuhamia upande mwingine.
Hayo yamesema Jumapili ya Februari 27, 2022 katika misa ya Jumapili na Padri Paul Mapalala Paroko wa Parokia ya Mtakataifu Maria Imakulata la Chamwino Ikulu, Jimbo Katoliki la Dodoma.
“Lakini jamani tuombeeni Ukraine na Urusi, si mmesikia Watanzania Wanarudiswa ehe, si ndiyo mmesikia? tuendeleea kabisa kuombea amani kwa namna moja au nyingine.”
Msomaji wa maombi wa misa hiyo ya jumapili, aliyaimba maombi matano huku mojawapo ya maombi hayo ni kwa ajili ya mataifa yajaliwe amani na haki ili watu wote waishi katika hali ya kufaana kwa ajili ya maisha yao.
Mwishoni mwa misa hiyo Padri Mapalala aliulizia juu ya hali ya Kolona kwa taifa letu huku akisema kuwa atawasiliana na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Chamwino ili kupata kibali cha kufanyika kwa misa za jioni ambazo ziliondolewa kwa sababu ya ugonjwa huo.
Wakati wa mahubiri ya misa hiyo Padri Mapalala alimshukuru Katekista Winfreyi Magawa ambaye amestaafu kazi hiyo na alikabidhiwa zawadi kadhaa ikiwamo nyumba, fedha tasilimu na vifaa kadhaa vya matumizi ndani ya nyumba hiyo.
Misa hiyo ilikuwa na waamini wengi ambapo walilijaza kanisa hilo huku wengine wakiwekewa viti nje.
Hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu kwa juma zima ilikuwa ya mvua za wastani, nalo jua likiwaka vizuri, huku mahindi yaliyopandwa yakiwa na urefu kati ya sentimenta 20-50.
Mwandishi wa taarifa hii alishuhudia baadhi ya waliojaliwa kulima wakichuma mboga mboga kadhaa za majani katika mashamba yao na wengi wao wamelima kilimo mseto.
0 Comments