Header Ads Widget

VITUO VYA HUDUMA YA PAMOJA VYATAKIWA KUANZISHWA KILA MKOA

 


MIKOA yote  nchini imetakiwa kuanzisha vituo vya huduma ya pamoja (one stop center) ili kurahishia utoaji huduma kwa wananchi wenye mahitaji ya huduma mbalimbali za kimaendeleo.


Hayo yalisemwa na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Innocent Bashungwa alipotembelea Shirika la Elimu Kibaha (KEC) kutembelea miradi ya maendeleo na uendeshaji wa shirika hilo.


Bashungwa alisema kuwa serikali imeweka mazingira mazuri ya utoaji huduma kwa wananchi hivyo kila mikoa lazima ianzishe vituo hivyo.


Amesema amefurahishwa na mkoa wa Pwani kuanzisha kituo hicho ambapo huduma za taasisi wezeshi na mamlaka mbalimbali zinapatikana hapo.


"Huduma bora kwa wateja kuzisogeza kwenye kituo cha huduma kwa wateja ambapo yale ambayo yanaweza kutatuliwayanatatuliwa,"amesema Bashungwa.


Amesema kuwa yale yanayoweza kutatuliwa kwa njia ya simu au kidigitali fomu zinakuwa kwenye mtandao.


Aidha amesema kuwa amefurahishwa na mkoa wa Pwani kwani taasisi zinazofuatwa mfano Brela TBS, TRA, Tanesco, Zimamoto, Uhamiaji zote zinapatikana sehemu moja.


Kila mkoa unapaswa kufanywa hivyo na kila mkoa kupitia kwa wakuu wa mikoa yote wafanye hivyo.


Naye Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha KEC Robert Shilingi alisema kuwa wameomba kibali cha msajili wa hazina ili kuruhusu kutumia ardhi ili kuanzisha miradi ya kimaendeleo.


Shilingi alisema kuwa miradi hiyo ni pamoja na uanzishaji wa bustani ya wanyamapori ambapo leseni tayari wameshaipata na ukumbi wa mikutano.


Shirika hilo lilianzishwa mwaka 1970 kwa sheria ya mashirika ya umma na lilianza kama mradi wa nchi za Nordic mwaka 1963 na ulikuwa mradi pekee barani Afrika na ulikabidhiwa kwa Mwalimu Julius Nyerere na Mfalme wa Denmark.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI