Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamewatembelea na kutoa zawadi kwa wanawake waasisi wa Chama hicho katika kata ya njoro manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utoaji wa zawadi hizo Katibu wa UWT wilaya ya Moshi Bi.Shakila Bakari Singano amesema kuwa amesema kuwa wameamua kutoa zawadi hizo kwa waasisi hao kwa kuadhimisha miaka 65 ya Chama Cha mapinduzi yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni lakini wao wameamua kuadhimisha Leo kwa njia hiyo.
Amesema kuwa wameamua kutoa zawadi kwa waasisi hao lengo likiwa ni kuazimisha miaka 45 ya Chama hicho ambayo yanatarajiwa kuazimishwa rasmi kimkoa tarehe Tano February mwaka huu.
"Tumetembelea hapa njoro tukiwa na vitu vya aina tofauti kwanza tumekuja kufanya usafi katika zahanati ya njoro na bà ada ya hapa tunaenda kuonana na waasisi ,ambapo Kila mmoja tunawaletea sabuni na sukari .
Hata hivyo ameiomba Serikali kuongeza fedha za mikopo inayotolewa na halmashauri kwani Wanawake Wana uwezo wa kukopa na kurudisha kwa wakati.
Amesema kuwa wanawake waliowengi ni wafanyabiashara na mitaji yao ni kubwa hivyo wanahitaji fedha za kuendeleza bishara hizo.
0 Comments