Header Ads Widget

TARURA NAMTUMBO YAENDELEE NA UJENZI WA BARABARA NA MADARAJA.

 




NA AMON MTEGA,_NAMTUMBO.


WAKALA wa baraabara Vijijini na Mijini (TARURA)Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wameendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe na ujenzi wa madaraja ambapo bajeti ya 2021/2022 wameweza kutumia kiasi cha sh. 754,927,477.28 sawa na asilimia 64 ya bajeti kutoka bodi ya mfuko wa barabara.


Akizungumza  ofisini kwake meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi Fabian Lugalaba amesema kuwa mwaka wa fedha 2021/2022 walitengewa bajeti ya kiasi cha sh. Bilioni 1.1 kwaajiri ya matengenezo ya barabara na utawala.


Amesema kuwa walipokea kiasi cha sh. Milioni 500 kutoka mfuko wa Jimbo na sh. Milioni 307.9 fedha kutokana na tozo hivyo wameweza kujenga madaraja pamoja na matengenezo ya barabara kwa kuweka mifereji.


Amesema kuwa bajeti ya 2022/2023 watafungua maeneo ya kilimo na shughuli za kijamii ,kukamilisha miradi viporo na kuboresha barabara zilizo kwenya hali nzuri ili zisiharibike na kurudisha nyuma hali ya upatikanaji wa barabara unaoweza kusababisha gharama kubwa ya matengenezo .


Hata hivyo mhandisi Lugalaba amesikitishwa na tabia ya baadhi ya wananchi wanaopenda kufanya shughuli za kilimo kando kando ya barabara na kuziba mifereji inayotoa maji hivyo kusababisha uharibifu wa barabara na kwamba amewaomba viongozi wa maeneo husika kutoa elimu kwa wananchi faida ya kulinda na kutunza miundombinu hiyo.




Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameipongeza serikali kupitia TARURA wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuhakikisha miundo mbinu ya barabara inapitika kipindi chote na hasa maeneo ya vijijini ambapo hapo awali kabla ya TARURA kuwepo hali ilikuwa mbaya maeneo mengi mawasiliano yalikatika na wananchi wengi kukosa huduma muhimu kama za matibabu lakini pia kupeleka mazao sokoni.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS