Header Ads Widget

TANESCO IRINGA WAANZA OPARESHENI UNGANISHA UMEME WATEJA WAPYA

 


SHIRIKA  la  umeme  Tanzania (TANESCO )  mkoani Iringa  limeanzisha  oparesheni maalumu ya  kuwawaingizia  umeme wateja   zaidi ya 2170  ambao  walilipia  gharama ya  Tsh 27000 kabla ya gharama mpya  za  umeme  kutangazwa .


Afisa  mahusiano  wa  TANESCO mkoa wa  Iringa  Francis  Mbwele alisema  kuwa  zoezi  hilo linatekelezwa  na  kikosi kazi   kilichoundwa na TANESCO  mkoa  wa Iringa kutoka wilaya ya  Mufindi , Kilolo na Iringa  ili  kuhakikisha  wateja wote  walioomba huduma ya  umeme  wanaingiziwa  umeme  kabla ya Machi 31  mwaka  huu.

“ Tunachokifanya  sasa ni  kutekeleza  agizo  la  serikali  la  kuhakikisha kabla ya  Machi 31 mwaka huu  wateja  wote  wawe  wameunganishiwa  umeme na baada ya zoezi hilo  kumalizika  TANESCO  mkoa  wa Iringa  imejipanga   mteja  wake mpya baada ya maombi  ya  kukamilisha  kujaza fomu  ndani ya  wiki  mbili atakuwa ameunganishwa na huduma ya  umeme”alisema

Alisema  kuwa  idadi  kubwa ya  wateja  ambao waliomba  umeme  ilikuwa Iringa mjini na Kihwele  ambako  TANESCO  imepeleka  kikosi kazi cha  kukamilisha uingizaji  wa  umeme  kwa  wateja  wake na  baada ya  kumaliza huko  kikosi  hicho  kitaelekeza  nguvu  zake  maeneo  mengine  ili  wateja  wote  kupata  huduma  hiyo kama walivyo omba.

Alisema kuwa   changamoto  iliyokuwa ikikwamisha  wateja  kuunganishwa   umeme kwa  wakati  ilikuwa ni upatikanaji wa vitendea kazi ambavyo  kwa  sasa  vipi vya  kutosha na  wana uhakikia  mkubwa  wa  kutekeleza majukumu yao  kwa  wakati .

Alisema  kuwa  upungufu  wa vifaa ulisababishwa na ongezeko  kubwa la  wateja   wa  umeme  ambao  walijitokeza  kwa wingi  baada ya  gharama ya  kuingiza  umeme  ilikuwa  ya  chini  zaidi mjini na vijijini ila kwa  sasa  kasi ya wateja  wapya siku  kubwa  sana imerejea ile ya  awali  ambayo  wana uhakika mkubwa wa  kufikisha  huduma hiyo kwa  wakati  zaidi .

Hata  hivyo Mbwele  aliwataka   wananchi  wanaohitaji   huduma ya  umeme  kuendelea  kujitokeza  kwani uhakika wa  kuunganishwa na umeme  upo  mkubwa na ndani ya muda  mfupi baada ya maombi  mteja  atakuwa ameunganishiwa  umeme.


Kwa  upande  wake  mhandisi  mkuu  wa TANESCO  mkoa wa Iringa Twaha  Kisaka  alisema   kuwa  tayari  serikali imetoa  muda  wa  kukamilisha  zoezi hilo la  ndio  sababu ya  kutengeneza   timu  za  kazi ili  kukamilisha zoezi hilo  ambapo   timu  13  zimeundwa  na kila timu kwa  siku  itatengeneza  service line 20  kwa simu na  kwa  timu  13  watajenga  zaidi ya service line 200.

Alisema  kuwa  wateja  wote  wanaoingiziwa  umeme  halina  gharama  mpya  kwa  wale  ambao  walilipia  kiasi cha  shilingi  2700 wataingiziwa kwa  gharama  hiyo  hiyo ambayo   walilipia wakati  huo hakutakuwa na gharama  mpya  na  wale  wanaoendelea  kulipia  kwa  gharama  mpya   nao  watafikishiwa  umeme   kulingana na walivyolipia.

Mteja  mpya  wa  umeme  mkazi  wa Kitwiru Iringa Amina Sanga  alisema  toka  mwaka 2021  alipohamia katika makazi yake  mapya  eneo  hilo hakuwa na  huduma ya  umeme na  kuwa zoezi hilo la  kuanza  kuwaingizia  umeme  wateja  wapya kwake ni  fursa  kubwa .

Hivyo  alilishukuru  shirika la umeme kwa kazi hiyo  nzuri  ya  kuwafikia  wateja  wake  wapya na  kuwa  kufikishwa kwa   huduma  hiyo ya  umeme  ni  mwanzo mwema  wa wananchi  kukuza kipato  chao  kwa  kuanzisha   shughuli za  uzalishaji  kupitia  umeme.

Mary  Kususange mwenyekiti  wa  mtaa wa Kitwiru  B  pamoja na kupongeza TANESCO kwa  oparesheni  hiyo  ya  kuwaingizia  umeme  wateja  wapya  bado  aliomba  utekelezaji  wa zoezi hilo  uwe   shirikishi kwa  wenyeviti  wa mitaa ili  waweze  kuwaonesha  maeneo  yenye  uhitaji mkubwa wa umeme.

Alisema  mtaa wake  una maeneo  ya pembezoni  zaidi  ambayo wananchi  wake  bado kufikiwa na nguzo  za  umeme  hivyo  kutokana  na  bei mpya ya  umeme TANESCO  waangalie  uwezekano wa  kusogeza  nguzo jirani na makazi ya  wananchi hao  ili waweze  kuingiza  umeme .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI