Teddy Kilanga _Arusha
Mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dkt.John Pima amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 Jumla ya vyanzo vya mapato 192 zimefanya vizuri na 54 havikufanya vyema kutokana na changamoto ya masuala ya usimamizi.
Akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya pili ya mwaka 2022,Dkt.John Pima alisema masoko yaliyofanya vizuri katika kiwango cha asilimia 89 kwenye ukusanyaji wa mapato ni NMC,Kijenge,Soko kuu, pamoja na Kilombero.
Aidha Dkt.Pima alisema vyanzo vya mapato ambavyo havijafanya vizuri ni pamoja na ukusanyaji wa ushuru wa mazao ya kahawa,ushuru wa maua kwani maeneo hayo hadi kipindi cha mwezi Desemba hayakufanya vizuri pamoja na gawio la Arusha meat,choo cha kilombero na kituo cha clokoni.
"Maeneo mengine ambayo hayakufanya vizuri pamoja na ada ya kunyonya maji machafu,upande wa chanzo na usajili wa magari wa kulipa vyakula ikiwa vyanzo hivyo vitatolewa taarifa katika baraza la robo inayofuata ili kuonyesha hatua iliyochukuliwa,"alisema Dkt.Pima.
Dk. Pima alisema kamati ya fedha inaendelea kuchukua hatu hadi kufikia februari 23 wako kwenye asilimi 66 ya uchumi wao ambapo kwa miezi inayofuata watafikia asilimia 100 na watahakikisha wanafanya vizuri.
Pia alisema kwa upande wa greda la halmshauri hiyo linaendelea na kazi na sasa limepangiwa katika kata zilizoandaliwa na Mhandisi wa jiji juu ya kufanya kazi kulingana na madiwani waliopeleka maombi katika halmashauri hiyo.
Alisema wamejipanga katika kuhakikisha jiji hilo linasonga mbele hivyo nawaomba wananchi wa jiji la Arusha kuendelea kuwa na ushirikiano katika masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo usafi hivyo anatoa rahi kwa watu wa daladala kuzingatia utunzaji wa mazingira.
Iranqe alisema wasifanye magari yao kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira kwa kutupa takataka hivyo ni vyema kila mmiliki wa gari ya usafiri akaweka sehemu ya kuhifadhia takataka ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wake Meya wa jiji la Arusha,Maximilian Iranqe alisema jambo la kukusanya mapato katika halmashauri ya jiji hilo wamekubaliana kuhakikisha katika robo ya mwaka inayokuja yanaongezeka ili kuweza kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Niwapongeze wataalamu wa jiji la Arusha kwa kuifanya kuwa ya pili katika makusanyo ya mapato kwenye kipindi cha fedha cha mwaka 2021/202 ikiwa wao ndio watendaji wakuu wa kila siku,"alisema Iranqe.
Sambamba na hilo alisema kwenye sekta ya elimu walishika nafasi ya kwanza miongoni mwa halmashauri 184 zilizopo nchini lakini kwenye suala la usafi pia walikuwa wapili nyuma ya jiji la Tanga hiyo wanafanya vizuri.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo,wamemuomba Mkurugenzi kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi za maduka yanayomilikiwa na jiji hili ili yapate wapangaji na kusaidia kuongeza mapato hapa yaliyopo maeneo ya Rangers.
0 Comments