Header Ads Widget

SERIKALI YAOMBWA KUPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA UCHIMBAJI WA MADINI MAENEO YA KWEMASHAI NA MAGAMBA LUSHOTO

 



Na Ibrahim Kunoga Tanga.

Mbunge wa Lushoto Mh  Shabani Shekilindi ameiomba serikali kupiga marufuku uchimbaji wa madini katika maeneo ya Kwemashai na Magamba  katika wilaya ya Lushoto.


Kauli hiyo ameitoa katika kikao  cha bajeti cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Tanga.


Mh shekilindi ametaka kikao hicho kiamuae na kupiga marufuku  maeneo hayo madini yasichimbwe ili kuokoa mazingira na kuomba watoa leseni wasitishe kutoa leseni.


Pamoja na hayo mh shekilindi amesema kuna maeneo yanaitwa madhahabu ambapo watu wanachimba dhahabu kwenye vyanzo vya maji hali inayopelekea watu waishio mabondeni kukosa maji.


"Mimi ushauri wangu maeneo Yale yasitishe kabisa yasichimbwe madini kwa sababu yakichimbwa milima itaporoka na yapo maeneo hatarishi ikiwemo shule na makazi ya watu;Amebainisha Mh Shekilindi.


Kutokana na kutegemea vyanzo vya maji vinavyotoka maeneo hayo Mbunge huyo amesema kwa sasa vita vya tatu vitakavyotokea vya athari ya dunia itakuwa  ni maji .


Pia amesema kwa sasa maeneo mengi lushoto watu wamechoma misitu  lakini maeneo hayo hayajawahi kurudishiwa miti na kuomba wataalam walishughulikie ili mapato yaongezeke na mazingira yaweze kuboreshwa.


Sambamba na hayo amesema pia wilaya hiyo umeme unahitajika sana kuboreshwa ili kuongeza mapato na kusema kuwa wananchi wengi wa lushoto wanategemea umeme ndio maana huwezi kukuta nyumba ya nyasi kwa hiyo umeme utakapofika vijijini tayari mapato ya halmashauri yataongezeka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI