Header Ads Widget

SERIKALI BORESHENI MASLAHI YA WATUMISHI KUZUIA UFISADI

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma 


MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh na aliyekuwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali amesema ili kutokomeza ufisadi serikali na Taasisi binafsi zinatakiwa kuangalia na kuboresha Maslahi ya watumishi wao. 


Ameyasema leo jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Taasisi za Umma na Binafsi kuweza kudhibiti ufisadi katika maeneo yao.


"Ni ukweli kuwa mishahara ya watumishi ni midogo na mtumishi anyeishi maisha ya kawaidi akisema aishi kulingana na mshahara huo bila kujishughulisha lazima mtu atafute njia za mkato ili kufanikisha na kutunza familia inayomtegemea," amesema 


Na kuongeza kusema " Serikali iangale upya mishahara ya watumishi wakati wengine watu au watumishi wanalazimika kuvunja sheria na kujiingiza katika vitendo vya rushwa kutokana na Maslahi," amesema Mkurugenzi huyo Utouh


Aidha amesema  katika nchi ya Tanzania Ufisadi  upo na Rushwa ipo ambapo ameeleza  jamo hilo limekuwa likiitesa dunia kwani ufisani unaumiza uchumi wa nchi na kuchelewesha maendeleo ya nchi na wananchi wake.


Kwa upande wake Ancletus Mhidze kutoka Idara ya ukaguzi wa ndani daraja la kwanza akimuakilisha Mkaguzi wa Ndani Mkuu Serikali amesema ufisadi umekuwa ukitokea katika miradi mikubwa ya kimaendeleo na wakaguzi wa ndani wameonekana kutofanya kazi zao ipasavyo nikutokana na ufinyu wa bajeti na vitendea kazi.


"Naiomba serikali kuwepo na bajeti ili wakaguzi wandani waweze kufanya kazi zao ipasavyo na kuweza kufichua na kuzuia mambo ya rushwa kwani vitengi vya ukaguzi wa ndani bajeti ndogo.



Naye Shakibu Mussa Nsekela Bingwa katika masuala ya Ubadhilifu Kudhibiti Rushwa na Ufisadi amesema Madeni hewa yanachangia kwa kiasi kikubwa ufisadi Tanzania na ili kuweza kusonga mbele  wanaopewa nafasi ya kusimamia watu na miradi watende haki  kwenye miradi fedha zitumike na miradi ionekane.


Hata hivyo amesema madeni hewa yataweza kuondolewa kwa wananchi kuongeza uwazi uwaminifu na uhadilifu kwa watumishi wa umma pale wanapokuwa wanasimamia malipo au wanapotoa malipo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI