Header Ads Widget

RAIS SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA MARIDHIANO DAY




 


Na Hamida Ramadhan, Dodoma



RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya MARIDHIANO DAY  yanayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 3 Machi mwaka huu 2022 mkoani Dodoma .


Hayo yamesema leo Jijini hapa na Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Dkt Alhad Mussa Salum wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya maadhimisho ya siku hiyo ya Maridhiano day.


Amesema katika siku hiyo wanamaridhiano wa Nchi nzima wamekubaliana kuadhimisha kwa uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto ,watu waliopata ajali na wagonjwa mbalimbali zoezi litakalo fanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convection Centre Dodoma .


" Katika wiki hii tumekuwa tukichangia damu katika maeneo mbalimbali ili kuoeleka takita hospitali zetu na siku hiyo ya tarehe 3 tutaweza kutoa idadi ni kiasi gani au chupa ngapi za damu tumeweza kuchangia wanamaridhiano," amesema Shekhe Salum.


Aidha amesema Jumuiya hiyo inaundwa na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali hapa nchini ambapo kazi kubwa inayofanywa na jumuiya hiyo ni kuhimiza amani na utulivu kwa watanzania bila kujali dini,jinsia rangi wala itikadi za kiasiasa.


"Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma na wadau wa amani kujitokeza kwa wingi na kuja kujumuika pamoja na wana maridhianao ili kuadhimisha siku hiyo ya MARIDHIANO DAY ambapo viongozi mbalimbali wa serikali watashiriki kwenye Maadhimisho hayo ,"amesema Shekhe Salum.


Hata hivyo ameitaja  kauli mbiu katika Maadhimisho hayo  kuwa ni "Tanzania nchi yetu komesha mauaji dumisha upendo, amani na utulivu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI