Header Ads Widget

ANASWA NA MKIA WA TWIGA BABATI

 



Mtuhumiwa wa ujangili Idd Ally Idd   mkazi wa kijiji cha  Mamire , wilaya ya Babati, mkoa Manyara amekamatwa akiwa na mkia wa Twiga baada ya kudaiwa kuwinda twiga na kuuza nyama kwa wananchi.


Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika operesheni za kupambana na majangili, katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Taifa ya Manyara- Tarangire na inayofanywa na kikosi maalum ambacho kinachoundwa na askari wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori(TAWA) askari wa burunge WMA , na askari wa Chemchem association ambao wameweza eneo la burunge WMA.


Akizungumza na waandishi wa habari Afisa wa kikosi cha kupambana na ujangili wa TAWA ambaye anaratibu Operation eneo hilo Pius William amesema tayari mtuhumiwa huyo amekabidhiwa polisi


"nikweli tumemkamata huyo mtuhumiwa na tayari mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa taratibu za  kumfikisha mahakamani zinaendelea kufanyika  "amesema


Akizungumzia kukamatwa mtuhumiwa huyo meneja wa Taasisi ya chem chem, Walter Pallangyo  amesema kukamatwa mtuhumiwa huyu ni mkakati kudhibiti ujangili unaoendelea.


"Askari walikuwa wanafatilia kwa muda  taarifa za  mtuhumiwa huyo ndipo waliandaa mtego uliofanikiwa kumkamata akiwa na mkia "amesema


Kikosi maalum kupambana na ujangili katika wilaya ya Babati kwa miezi minne sasa kimekamata watuhumiwa watano wa ujangili,wakiwepo waliokutwa na meno na tembo na nyara za serikali ikiwepo ngozi za pundamilia.


Watuhumiwa hawa  wakikamatwa Katika operation ambazo zinaendelea kutokea kwenye eneo la hifadhi ya wanyamapori ya jamii ya Burunge, ambayo ipo katikati ya hifadhi za Tarangire na Manyara.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI