Header Ads Widget

WAZIRI DKT. NDUMBARO AONGOZA MAKAMPUNI ZAIDI YA NANE YA KITANZANIA KUNADI UTALII WA UWINDAJI NCHINI MAREKANI



 

NA MWANDISHI MAALUM, LAS VEGAS, MAREKANI.

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameyapongeza makampuni zaidi ya nane [8] ya Kitanzania yaliyopo Nchini Marekani kwa kazi nzuri ya  kuitangaza Tanzania kwenye sekta ya uwindaji wa kitalii  kwa kushiriki katika mkutano wa 50 wa mwaka  wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) 

 

Mkutano huo wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ulioandaliwa  na Safari International Club (SCI) umeanza  leo  na  unafanyika  katika Jiji la Las  Vegas, Nevada nchini Marekani

 

Akizungumza Jijini hapa, Dkt. Ndumbaro amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa Tanzania   yakiwemo Makampuni  na viongozi  wa Serikali  walioshiriki katika mkutano huo  kujifunza na kuinadi Tanzania katika masuala ya Uwindaji wa Kitalii katika  nyanja za Kimataifa 

 ''

'' Katika maonesho   haya zaidi ya makampuni 200 yanayofanya Biashara ya Uwindaji wa Kitalii kutoka kila kona ya dunia yapo hapa ikiwemo kutoka  bara la Ulaya, Amerika, Afrika, lakini nchi za Canada  na Marekani yenyewe'' Amesisitiza Dkt. Ndumbaro

 

Dkt. Ndumbaro amesema  maonesho  hayo  ni makubwa sana  ambayo yanatoa fursa kwa nchi  kujifunza sekta ya uwindaji wa kitalii kuwa ipo wapi sasa hasa kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO 19.’’ 

 

Ameongeza kuwa '' Mimi kama Waziri mwenye dhamana na Utalii najisikia fahari kuona makampuni zaidi ya 8 ya Kitanzania yapo hapa yakiiuza Tanzania kwenye sekta ya uwindaji wa kitalii. 

 

Dkt. Ndumbaro amesema Makampuni zaidi ya nane kutoka Tanzania kushiriki katika Mkutano huo ni hatua nzuri sana,  '' Huu  ni ushahidi tosha  kuwa Makampuni hayo yanafanya vizuri na yanakubarika Kimataifa  lakini pia tumechukua fursa hii ya kuweza kukutana nao kwa ujumla wake lakini pia mmoja mmoja kuweza kuzungumza nao na kubadilishana mawazo.’’ Alisema Dkt. Ndumbaro.

 

Amesisitiza kuwa Mazungumzo aliyoyafanya na Makampuni hayo  yamemfundisha mengi ikiwemo kuanza kuingalia sekta hii ya uwindaji wa kitalii  kwa namna   ya utofauti kabisa, na kwamba Uwindaji  ni sekta ya kipekee sana ambayo inaweza ikawa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kama itachukuliwa kwa uzito unaostahili

 

Tumekubaliana tutaendelea kujipanga kushirikiana na  kwa siku zilizobaki kuiuza Tanzania lakini muhimu zaidi kuongea na Waandaji wa maonesho haya na maonesho mengine ili katika safari ijayo Tanzania ishiriki kama nchi kwa umoja wake na kwa fursa kubwa zaidi ili kuuza utalii wa uWindaji'' Alisema Dkt. Ndumbaro


 

Kwa upande wake mmoja wa wanaoendesha biashara ya Utalii wa Uwindaji nchini Tanzania ambaye yupo kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya Michel Mantheakis Safari, Michel Manteakis amesema Maonesho hayo  wamekuwa wakihudhuria kila mwaka na kupata faida kubwa ya soko kutoka kwa wateja wanaofika kwenye mikutano hiyo.

 

"Mikutano hii ni muhimu sana kuhudhuria kwani tunakutana na wageni mbalimbali na bila kuhudhuria unakosa fursa kwani Mawakala (agent) na wateja wanafika hapa'' lisisitiza 

 

..Hapa kuna Washiriki wa kutoka nchi zote za Afrika hivyo  usipohudhuria Mkutano huu  utakosa soko. Hapa ndipo  tunapokutana na wageni wetu tunapata faida ya kuweza kuendesha safari zetu, wateja na Mawakala wanapata fursa ya kutufanyia usahili na pia wanaona jinsi  tunayonadi bidhaa zetu’ alisema Michael Mantheakis.

 

 

Mkutano huo umeanza  rasmi tarehe 19 Januari, 2022 na kufunguliwa rasmi tarehe 21 Januari 2022 katika Jiji la  Las Vegas, Nevada nchini Marekani ukiwa na lengo ya kuwakutanisha watunga sera na wafanya maamuzi katika ngazi  za juu kutoka nchi  mbalimbali duniani kuweza kujadili masuala ya kisera katika kuendeleza sekta ya uwindaji.

 

Katika Mkutano huo, Dkt. Ndumbaro anazinadi fursa za uwekezaji za uwindaji wa kitalii zilizopo nchini  Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Matajiri wakubwa duniani kuchangamkia uwekezaji huo uliopo nchini Tanzania

 

Kupitia Mkutano huo Tanzania itaweza kuongeza uelewa zaidi katika masuala ya kisera na maamuzi katika kuendeleza sekta ya uwindaji wa kitalii nchini


Katika msafara huo, Waziri Dkt. Ndumbaro aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali, Hamis Semfuko, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi,

 

Mwingine  ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF)  Lulu Ng'wanakilala pamoja na Afisa Mhifadhi Mkuu wa Wanyamapori wa kutoka TAWA, Segolin Tarimo

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI