Header Ads Widget

MATAIFA 55 KUSHIRIKI MBIO ZA KILL MARATHON FEBRUARY 27

 



Mkoa wa kilimanjaro unajiandaa kupokea ugeni kutoka ndani na nje ya nchi watakaokuja kushiriki Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, (kili marathon) zinazotarajiwa kufanyika  Februari 27, 2022,  mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).


  Aidha mkoa upo Katika  maandalizi ya kupokea wageni kutoka nchi  55 watakaoshiriki Mbio hizo zilizoandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na kuratibiwa na wadau kampuni ya Executive Solutions Limited .


Akizungumza katika uzinduzi wa Mbio hizo Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Steven Kagaigai amesema kuwa timu ya usalama ya mkoa imejipanga kuhakikisha kuwa watu watakaokuja kushiriki mbio hizo wanakuwa salama .


"Lakini ninavyosema mashindano haya kwetu sisi ni uchumi kwa sababu nadhani tutafanya biashara nzuri tu make watu elfu kumi na nne kwa mkupuo,wauzaji watauza na hoteli zote zimeshajaa"Alisema Kagaigai.


Amesema kuwa Mbio hizo ni muhimu ambapo amesema mbali na mbio hizo za kimataifa kufanyika mkoani Kilimanjaro Bado Kuna uhaba wa uwanja wa michezo utakaowabeba watu wengi ambapo amesema uhitaji wa mkoa ni kuwa na uwanja mzuri wa michezo .


Hata hivyo amewataka wadau wa maendeleo pamoja na viongozi kushikamana kwa pamoja ili kuangalia eneo ambalo  uwanja wa michezo utskuwepo.


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi, ambaye pia ni Meneja wa Chapa ya Grand Malt, alisema maadhimisho ya 20 ya mbio za Kilimanjaro marathon ni mafanikio makubwa haswa ikitiliwa maanani ya kuwa Kilimanjaro premium lager imekuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo tangu kuasisiwa kwake miaka 20 iliyopita.


“Mbali na kuwa mashindano ya kimataifa yaliyojijengea umaarufu mkubwa, sisi kama wadhamini wakuu pia tumehamasishwa kujitolea zaidi kutokana na mbio hizo kuchangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa sekta ya utalii na utamaduni wa Mtanzania kwa ujumla”, alisema 


Alisema wao kama wadhamini wakuu wamejipanga vyema kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambayo yatahusisha matukio ya kusisimua katika wiki nzima ya kuelekea mbio hizo ambapo alisema jumla ya shilingi milioni zimetengwa kwa ajili zawadi.


Irene aliendelea kusema kuwa washindi wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake kwa mbio za kilomita 42 watazawadiwa shilingi milioni 4 kila mmoja na kwamba Mtanzania mwanamume au mwanamke atakaeshika nafasi ya kwanza katika mbio za kilomita 42 atapata zawadi ya ziada ambayo alisema ni motisha ya Tsh 1.5 m kila mmoja.


Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema: “Sisi tukiwa ni wadhamini wa mbio za kilomita 21, maarufu kama Tigo Kili-Half marathon kwa zaidi ya miaka 7 sasa, tunatarajia mbio za mwaka huu zitakuwa ni za kusisimua, ambapo tunatarajia washiriki zaidi ya 5,000 kutoka ukanda mzima wa Bara la Afrika kutokana na kuongezwa kwa thamani ya zawadi za washindi”.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI